ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 25, 2013

VYAKULA HIVI HUDHANIWA NI SALAMA, LAKINI SIYO!



KUNA vyakula vingi ambavyo vimekuwa vikitangazwa kibiashara kuwa ni bora kiafya lakini siyo kweli. Baadhi ya vyakula hivyo vinaelezwa katika makala haya kama ifuatavyo:

NYANYA ZA KOPO
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, vyakula vingi vya kwenye makopo huwa na kiwango kingi cha kemikali aina ya BPA ambayo imegundulika kuwa na uhusiano wa magonjwa ya saratani ya matiti na kibofu cha mkojo, ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa moyo na matatizo ya kuzaa watoto wenye kasoro kiakili au kimwili.
Ili kujiepusha na hatari ya kupatwa na madhara hayo, watu wanashauriwa kuacha kutumia nyanya za kopo na vyakula vingine na badala yake watumie nyanya asilia. Iwapo hapana budi, nyanya au chakula kingine cha kusindika kinachoweza kutumiwa ni kile kilichohifadhiwa kwenye chombo aina ya ‘glasi’ na siyo ‘bati’.

NYAMA ZA KUSINDIKA
Ukweli ni kwamba, nyama za kwenye makopo nazo si salama kiafya na zinatakiwa kuepukwa kabisa na hii ni kwa mujibu wa utafiti wa kitabibu uliofanywa mwaka 2011 kwa stadi 7,000, uliochunguza uhusiano kati ya ugonjwa wa saratani na nyama.
Imeelezwa kuwa utafiti huo ulifanywa na Mfuko wa Dunia wa Utafiti wa Saratani kwa kutumia fedha za walipa kodi, ikiwa na maana kwamba utafiti huo haukuegemea upande wowote, ulikuwa huru na wa haki. Hivyo matokeo ya utafiti wake ni ya kuaminika.
Utafiti huo umetoa ushahidi mkubwa kuwahi kutolewa na umethibitisha matokeo ya tafiti zilizowahi kufanywa zikielezea kuwa nyama za kwenye kopo au nyama za kusindika huchangia hatari ya mtu kupata saratani, kiasi chochote utakachokula unahatarisha afya yako, hata kama ni kidogo.
Hivyo kama wewe ni mpenzi wa nyama, basi kula nyama ya kawaida na ile itokanayo na ng’ombe wa ‘kiswahili’ ambao hufugwa kwa kula nyasi asilia. Na siyo nyama ya wale ng’ombe wanaolishwa nafaka na madawa ya kuwafanya wanenepe na kutoa maziwa mengi. Vinginevyo jiepushe kabisa na ulaji wa nyama.

MAFUTA YA KUPIKIA
Miongoni mwa vyakula hatari tunavyoweza kuwa tunakula kila siku, ni vile vinavyopikwa na mafuta yaliyokwisha ondolewa virutubisho wakati wa kuyatengeneza.

Itaendelea wiki ijayo...

GPL

No comments: