ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 2, 2013

‘Zanzibar lazima iwe mamlaka yenye dola

Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad amesema muundo wowote utakaokuja wa Muungano lazima Zanzibar iwe na mamlaka kamili ya kidola.
Alisema kinyume na mamlaka kamili rasimu itakayokuja itakataliwa bila ya kigugumizi.
Maalimu Seif Sharif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUf) aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kibandamaiti Zanzibar.
“Wazanzibar wapatao asilimia 66 wametoa maoni yao yenye mamlaka kamili, leo uje na katiba inayokwenda kinyume na matakwa yao, hilo halikubaliki” alisema Maalim Seif.
Akizungumza juu ya mambo ambayo hayapaswi kuwa ya Muungano alisema ni pamoja na uraia, uhamiaji, sarafu, mipaka, polisi na mambo ya nje.
“Tanganyika watoe Pasi za kusafiria zao na Zanzibar zao” alisema Hamad.
Mapema mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu alisema hatarajii kama Tume ya Mabadiliko ya Katiba itapanga maoni ya vongozi wengi wa Juu Tanzania ya kuipa Zanzibar Mamlaka yake.

1 comment:

Anonymous said...

Nadhani itakuwa vyema Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili na italeta mafanikio kwa pande zote mbili Zanzibar na Tanganyika. kwa mfano, mambo ya nje kutakuwa na wawakulishi wawili ambao watasaidia kuleta Maendeleo kwa njia za misaada from nchi tajiri na Zanzibar itaweza kujitatua na kusaidia maendeleo na nchi. pili, kuwepo passport ni Jambo Jena sana, kwani itapunguza uingiaji mbovu wa watu kutoka nchi jirani ambao wanajifanya watanzania. kwa mfano sasa hivi wanachi wengi kutoka Kenya, Uganda, Zambia na nchi nyengine wanaingia Tanzania bila ya mpangilio maalum. kuna dimbwi la wizi kutoka nchi jirani ambao wanafanya uhalifu nchini kwetu bila kutambulikana wanatoka wapi. Kutakuwa na uamuzi mzuri kwa nchi zetu bila kuekeana vikwazo vya huyu ajiunge na upande upi kwamfano, kujiunga na OIC NA nchi nyengine. maovu ya kiholela yatapungua kwa pande zote mbili.