ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 13, 2013

DIASPORA WORLD CUP, BOSTON, MASSACHUSETTS TANZANIA YAITUNGUA LIBERIA 2-0

 Timu ya Tanzania
 Timu ya Liberia
 Makepteni wa timu zote mbili katika picha ya pamoja na waamuzi wa mpambano.
 Mchezaji wa Tanzania Rahim Chomba akimueka kibindoni mchezaji wa Liberia
Mchezaji wa Tanzania Francois jezi # 7 akimtoka beki wa Liberia na kuifungia Tanzania bao la 2.
Mchezaji wa Tanzania Dotto Mnyamuru akikubali yaishe kwa mchezaji wa Liberia

Timu ya Tanzania ilipeperusha vizuri bebndera ya Tanzania kwenye Diaspora World Cup katika mechi yao ya kwanza kwenye mashindano hayo yanayofanyika Boston kwa kuibamiza timu ngumu ya Liberia kwa bao 2-0 mabao ambayo yalifungwa kila kipindi.

Mchezo huo ilibidi uchezwe ddk 25 kila kipindi kutokana na timu ya Liberia kuchelewa kufika uwanjani hapo. Watanzania wakifikiri muamuzi wa mchezo angewapa ushindi wa chee lakini kabla muamuzi hajafanya hivyo timu ya Liberia iliwasili na ikaamuliwa mechi ilchezeshwe kwa dakika 50 ili kuweza kupata mshindi atakayesonga mbele. Mpaka kipenga cha mwisho Tanzania 2 Liberia 0.

No comments: