ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 3, 2013

FBI WAMKAGUA KOVA NA MBWA LICHA YA KUWA NA WAZIFA MKUBWA KATIKA JESHI LA POLISI TANZANIA

Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale, lakini hili la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo Kikuu.”
Dar es Salaam. Ofisa mmoja wa Usalama wa Marekani (FBI), akiwa na mbwa jana aliingia Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kufanya ukaguzi.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya msafara wa magari ya Marekani kupita yakitokea Ikulu kwenda Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kumlaki Rais Barack Obama.
Polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema ofisa huyo aliingia na mbwa hadi maeneo ya mapokezi, lakini muda mfupi walitoka.
“Walikwenda moja kwa moja mapokezi wakafanya ukaguzi, kisha wakatoka nje ya jengo na kama hiyo haitoshi, ofisa huyo akiwa na mbwa alikwenda sehemu ya kuegesha magari yenye kesi na yale ya kawaida na kuanza kufanya ukaguzi, baada ya hapo waliondoka,” alisema polisi huyo na kuongeza:
“Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale, lakini hili la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo Kikuu.”
Hata hivyo, usalama kwenye vituo vingi ikiwamo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusu Nyerere, vilikuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa makachero wa Marekani.

4 comments:

Anonymous said...

Kwani kabla Obama hajawasili nchini si tayari mliambiwa kanunu za ulinzi wa FBI na msafara mzima wa Rais Obama? Sasa inakuwaje mnalalamika mmedhalilishwa kwani wameivamia nchi si wamekuja kwa mualiko maalumu kutoka kwa Rais Kikwete? Sioni mnacholalamika kama kina uzito hata kidogo. Huyo ndo Rais wa Dunia bwana, na huo ndo ulinzi wake sasa sijui mnalalamika ili iwaje? Kwanza kasha ondoka hivyo endeeeeleni na maisha yenu ya kila siku. Ila naaamini mmejifunza kuwa wenzetu hao ulinzi kwao ni kitu cha maana na cha hali ya juu sana sana sana. Ninyie kazeni buti kiulinzi. Kaazi njeema.

Anonymous said...

Licha sio richa hivi anayeandika hizi habari ni nani awe makini maana hii ni lugha yetu inakuwa ni aibu kama huwezi hata kuiandika vizuri sasa sijui anakua na haraka ya post kabla ya kupitia makala yake

Anonymous said...

Mbona unalalamika? Au kwa kuwa aliwaingilia bila kufata taratibu zenu mlizojiwekea? Kwamba Kila aingiaye APo lazma awape hongo? Mngekuwa na sifa ya uadilifu na kufuata the rule of law wala hawa FBI wasingekuwa na wasiwasi nanyi.

Anonymous said...

Asante Mungu kwa kutupatia nafasi ya Obama kufika Tanzania. Kutokana na ujio wa Obama Tanzania, nafikiri umeonyesha kwa kiasi gani umuhimu wa kufuata taratibu na sheria. Kazi haichanganywi na kufahamiana. Si jambo la kunishangaza kuona kuwa mkuu huyo wa polisi amekaguliwa, si ajabu hii inatokana na mambo mengi ambayo idara hii ya polisi imeonyesha kutoyafuata. Iwe changamoto kwa Polisi ya kujiuliza kwanini wamemchunguza mkuu huyo wa polisi? badala ya kulichukulia kama kudhalilishwa.