ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 8, 2013

MBOWE AFANYA MAZUNGUMZO NA MAAFISA WA IKULU YA MAREKANI



Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alialikwa kushiriki dhifa ya Kitaifa Ikulu wakati wa ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani alifanya jambo kubwa muhimu kwa mustakabali wa Demokrasia hapa nchini.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Kiongozi Rasmi wa upinzani bungeni alipata fursa adhimu ya kufanya mazungumzo ya Faragha na maafisa wa Ikulu ya Marekani walioambatana na Rais Barack Obama.
Mpaka sasa kilichozungumzwa na Kiongozi huyo anayeongoza chama kinachopendwa na watanzania wengi zaidi hakijawekwa bayana ingawa wachunguzi wa mambo wanasema yalikuwa mazungumzo nyeti na muhimu kwa mustakabali wa demokrasia na amani ya Tanzania.
Taarifa zaidi zinasema Kiongozi huyo wa Upinzani nchini alialikwa na Ikulu kwa shinikizo kubwa kutoka ubalozi wa Marekani kutokana na Taifa hilo kutambua kazi kubwa inayofanywa na wabunge wa CHADEMA ndani ya bunge la Tanzania.

2 comments:

Anonymous said...

Kusema chadema ndio chama kinachopendwa na watanzania wengi ni kupotosha ukweli na ni kuonyesha udhaifu mkubwa ktk fani ya uhandishi wa habari

Anonymous said...

Hizi habari kuwa chama cha Chadema ndo kinapendwa na watanzania wengi nchini ni za kizushi na za kupotosha sana. DJ Luka kabla hujaposti kitu nakuomba upitie kwanza na kukielewa maana ungesema tu Mwenyekiti wa Chadema hukuwa na haja ya kulonga longa hayo mengine.Jamani maneo yakiandikwa ni lazima yawe na usahihi Fulani au ni bora yasiandikwe kabisa!!!!! Ni wazo tu.