ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 8, 2013

WAKAZI AMJIBU TID"BAADA YA KUMDISS ATAIMBA WIMBO GANI BBA"SOMA HAPA ALICHOSEMA

Rapper Webiro Wassira aka Wakazi amefunguka kupitia Bongo5 kuwa kitendo cha TID kumdiss kuwa haoni wimbo atakoutumbuiza kesho kwenye eviction show ya Big Brother Africa The Chase kinaonesha kuwa staa huyo wa ‘Kiuno’ hajui anachokiongea.
Jana kupitia Twitter, TID aliandika: Wakazi ataimba wimbo gani, anaenda kuonyesha kofia zake za marekani#mzee kasema#radarworththisshit#watuwabaya#msiwemaf**a.

Akijibu kuhusu kile anachoweza kujibu baada ya tweet hiyo ya TID, Wakazi amesema: Sasa ntamjibu nini, anaongea vitu asivyovifahamu, yeye hapo akimuona Wakazi anaona kofia za Marekani sasa mtu kama huyo utaongea naye!!”

“The greatest ignorance ya mtu ni pale anapoamua kudiss kitu ambacho hakijui au hajakifahamu bado vizuri , mtu kama huyo huwezi kuanza kubishana naye, na yeye ananiona mimi Mmarekani, wakati mimi ni Mtanzania, angekaa miaka mitatu Ulaya au Marekani angejiona na yeye ni mtu wa huko kwa jinsi upeo wake ulivyo.”

1 comment:

Anonymous said...

Big up wakazi.nimependa sana perfomance yako kaka.kwanza ulivaa vzr uliimba vzr na mashabiki wako ulienda nao vzr.haijalishi unaishi wapi lkn am so proud kuona kuna watanzania wanaoishi nje lkn wanathamini utanzania wao.achana na wanaojaribu kukulet down na wala usiwajibu wee kaza buti na fanya kazi.mix yako ya kiswahili na english mi niliipenda sana.kila la kheri wakazi.keep the flag high!