ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 2, 2013

PICHA NYINGINE YA ZIARA YA OBAMA ALIPOWASILI TANZANIA


Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Rais Obama wakitembea kwa pamoja.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Michelle Obama muda mfupi baada ya kuwasili kwa Rais Obama nchini kwa ziara ya siku mbili nchini.
Mhe. Rais Obama akiongozana na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange mara baada ya kukagua gwaride la heshima.
Mhe. Rais Obama akikagua Gwaride la Heshima
Mhe. Rais Obama na Mhe. Rais Kikwete wakisikiliza nyimbo za Mataifa yao zilizopigwa kwa Heshima ya Rais Obama.
Mhe. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete, Mama Michelle Obama na Viongozi wengine wa Serikali wakiwa Uwanjani hapo wakati wa mapokezi.
Mhe. Rais Obama akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mkewe Mhe. Mama Salma Kikwete na Mama Michelle mara baada ya kupokelewa.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana mchana.nyuma ya Rais na mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia
kwa picha zaidi bofya read more
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barack Obama wa Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Padu Ameir Kificho katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jana mchana.
Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama wakipokewa kwa shangwe Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akiwa ameambatana na mgeni wake, Rais wa Marekani, Barack Obama, wakati wakielekea kuzungumza na wanahabari Ikulu, jioni ya jana.
Raisi Barack Obama wa Marekani na Rais Kikwete wa Tanzania wakijibu baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano uliofanywa na Rais Obama na Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar jana mchana.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Freddy Maro-IKULU)

4 comments:

Anonymous said...

Safiiiii sana wakuu wamependeza sana. Kumeonekana upendo, furaha na utulivu wa hali ya juuu!!! Mungu ibariki Tanzania.

Pastor Johnson Kiulah said...

Hakika ilikuwa ni siku ya kipekee na ya kumbukumbu Tanzania kupata bahati ya kuupokea ugeni mzito wa ziara ya Rais Barack Obama. Hakika Tanzania na Marekani zinapendeza sana Mungu ibariki Tanzania, Marekani, Afrika na Ulimwengu kwa ujumla.

By Johnson M. Kiulah

Pastor Johnson Kiulah said...

Hakika ilikuwa ni siku ya kipekee na ya kubukumbu Tanzania kupata bahati ya kuupokea ugeni mzito wa ziara ya Rais Barack Obama. Ni ombi letu kuwa ziara hii iwe na manufaa kwa nchi zote Tanzania na Marekani. Mungu ibariki Tanzania, Marekani, Afrika na Ulimwengu kwa ujumla. Amina.

By Johnson M. Kiulah

Anonymous said...

Nimefurahishwa na ubora wa picha mpiga picha wako mpe promotion ya mchahara anastahili, pili nimependa ustaarabu wa blog yako uko juu, tatu watanzania tujivunie ujio wa ugeni huu ni fursa ya pekee Mungu ametupendelea.Wakenya wametamani sana fursa hii ukizingatia kuwa pres Obama ni mtu wao. Let us use this golden opputunity to raise our economy.