“Sasa nikawa najiona ninaanza kutokwa na vipele sehemu ya mbele na nyuma vinawasha sana na nimejikuna na sasa vimekuwa vidonda na vinatoa harufu kali.’ Mtoto wa miaka 15
Dar es Salaam. Mkazi wa Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpa mimba na kumwambukiza,Ukimwi mtoto wa umri wa miaka 15.
Pamoja na kumwambukiza magonjwa, mtuhumiwa pia anadaiwa kuharibu sehemu za siri na nyuma ya maumbile ya mtoto huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Amana.
Mtuhumiwa wa tukio hilo ni mlinzi wa minara ya simu, na inadaiwa kuwa alimshawishi mtoto huyo aliyekuwa anafanya kazi za ndani, aache kwa madai kuwa anamtafutia kazi yenye kipato kikubwa.
Akisimulia mkasa huo, katika Hospitali ya Amana alikolazwa, huku akitoa machozi, mtoto huyo alisema “mimi natokea Masasi mkoani Mtwara. Mama mmoja wa Mbagala alikuja kunichukua kwa ajili ya kumfanyia kazi za ndani lakini alinifukuza kazi akisema sijui kazi,”alisema na kuongeza:
“Nilihangaika na nikapata kazi za ndani kwa mama mmoja wa Gongo la Mboto ambako baba huyu mlinzi wa minara ya simu aliniambia niache kazi, niliyokuwa ninalipwa Sh20,000 na niende kufanya kazi yenye malipo ya Sh40,0000”.
Alidai kuwa baada ya kutoroka kwa aliyekuwa akimfanyia kazi awali, alihamia kwa mlinzi huyo aliyekuwa amepanga eneo la Vikongoro, Chanika iliyopo Manispaa ya Ilala na kukaa huko kwa madai atampeleka kwenye kazi hiyo.
Alidai uhusiano wao alipokuwa akienda sokoni na hata baada ya kuhamia kwake alilazimisha kumingilia kimwili na kinyume na maumbile. “Ikawa anafanya hivyo...kila siku akitoka kazini alikuwa ananilazimisha kufanya tendo la ndoa hivyo alikuwa ananiingilia mbele na nyuma na kunisababishia maumivu. Nikimwambia naumia ananitishia sin’topata hata hiyo kazi yenyewe” na kuongeza:
“Sasa nikawa najiona niko tofauti,nikaanza kutokwa na vipele sehemu ya mbele na nyuma vinawasha sana na nimejikuna na sasa vimekuwa vidonda hivi hapa (anamwonyesha mwandishi) hata mwenyewe unaona na vinatoa harufu kali”.
Akaongeza kuwa baada ya kuona vidonda vimezidi, kabla na baada ya kufanya tendo la ndoa anachemsha maji ya moto huku yakichanganywa na dawa kwa ajili ya kujikanda sehemu zilizoathirika.
Amesema licha ya kuathirika hivyo, mwanaume huyo alikuwa akimzuia kutoka nje ya nyumba hiyo na alikuwa akioga na kujisaidia kwenye chumba hicho hadi anaporudi kazini mwanaume huyo na kumwaga huku chakula akiletewa na wakati mwingine analala bila kula.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala , Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema, upelelezi haujakamilika na mtuhumiwa yupo kituo kidogo cha Polisi Stakishari kwa mahojiano zaidi. Ili kupata taarifa zaidi juu ya mkasa huu usikose kusoma Mwananchi Jumamosi.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment