MREMBO Sylona Nyameyo juzi
usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Temeke lililofanyika katika Ukumbi
wa TCC Changombe, jijini Dar es Salaam.
Sylona aliye mwanafunzi wa
mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akisomea mambo ya
sheria alifanikiwa kuwashinda warembo wengine na kufanikiwa kujitwalia taji
hilo.
Katika shindano hilo
lililokuwa na upinzani mkali, ulioambatana na burudani za kumwaga, ilishuhudiwa
nafasi ya pili ikienda kwa Marietha Boniface, ambaye naye ni mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUCHS).
Nafasi ya tatu ilikwenda
kwa Latifa Mohammed ambaye amemaliza kidato cha sita mwaka huu, hivyo warembo
hao kujihakikishia nafasi ya kuingia katika fainali za Redd’s Miss Tanzania.
Ushindani ulionekana
dhahiri katika shindano hilo, ambapo warembo walikuwa wakichuana mno, huku
mashabiki waliojitokeza hapo wakijikuta wakishangilia muda wote.
Akizungumza mara baada ya
kuvikwa taji hilo, Sylona alisema amefurahishwa mno na matokeo hayo na
atahakikisha hawaangushi wakazi wa Temeke katika shindano la Redd’s Miss
Tanzania.
“Nilijua toka mwanzo
lazima niwashinde, maana nilijiamini na niliona nina vigezo vyote, sasa ni
wakati wa kwenda kupambana katika Redd’s Miss Tanzania ili kurudisha heshima ya
Temeke,” alisema.
Shindano la Redd’s Miss
Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa
na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment