Advertisements

Sunday, July 28, 2013

WATUHUMIWA WALIOKAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA CHINA NA HONG KONG WAFUNGUKA NA KUANZA KUWATAJA WAKUBWA WAO


Mbunge Wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania kutoka jimbo la Kinondoni, inasemekana ametajwa na wafungwa wa kitanzania waliofungwa jela huko nchini Hong Kong kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya.

Taarifa hiyo iliyomhusisha Mbunge huyo na mtandao huo mkubwa wa biashara hiyo ya madawa ya kulevya nchini Tanzania, ilitolewa katika barua maalum iliyoandikwa na mmoja wa Wafungwa katika magereza ya nchini Hong Kong ambapo inasemekana kuna wafungwa wa kitanzania wanaofikia 200.

Kati ya hao wafungwa 200 waliopo magerezani na vizuizini, 130 tayari wameshahukumiwa na 70 bado wanasubiri kesi zao kutajwa. Kuanzia Mwezi wa Tano mpaka wa Sita mwaka huu wa 2013, tayari Watanzania wapatao 50 wameshakamatwa na madawa ya kulevya wakati wakijaribu kuingia katika viwanja vya ndege vya nchi za China na Hong Kong.

Mbali na Hong Kong, pia kumekuwepo na taarifa mbalimbali za raia wa Tanzania ambao wamekatwa na madawa ya kulevya nchini Afrika ya Kusini na kwingineko duniani. Mmoja kati ya waliokamatwa na madawa hayo ni mwanadada mahiri wa Kitanzania ambaye alikuwa mrembo katika video mbalimbali za Bongo Flava anayeitwa Agnes Gerald au kama anavyojulikana na wengi kwa jina la Masogange.

Waraka huo wa mfungwa huyo wa Kitanzania pia umeorodhesha idadi kubwa ya wafanyabiashara wengine nchini Tanzania ambao ni wahusika wakubwa katika biashara hii haramu ya madawa ya kulevya.
Madawa hayo ya kulevya yanasemekana yanaingizwa nchini Tanzania kwa wingi kwa njia ya meli na boti mbalimbali yakitokea katika nchi za Pakistan, Afghanistan na nchi nyingine za Mashariki ya mbali.
Ni muhimu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha kampeni kubwa ya kuwakamata wahusika wote katika biashara hii na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, athari za madawa hayo zimezidi kuonekana sehemu mbalimbali nchini Tanzania na dunia nzima.
Soma barua iliyowataja wafanyabiasha hao wakubwa wa madawa ya kulevya nchini Tanzania hapo chini.




Kama ni kweli haya sasa ni majangazzzzzzzzzzzzz haswa.

4 comments:

Anonymous said...

Ndg uliyetoa taarifa hiyo unastahili pongezi kwani ni wachache wanaoweza kukiri kuhusika na biashara hii haramu kama ulivyofanya wewe. Pongezi kwako kwa kutoa orodha ya baadhi ya drug barons hapo Tanzania. Hii itasaidia kuufuatilia huo mtandao. Ombi langu kwako itakuwa vizuri kama utaikamilisha orodha hiyo kwa kuwataja hao wengine hata kama ni wakubwa kiasi gani kwani jamii itawajua na vyombo vya dola vitumike kuwashughulika. Kwa mara nyingine pongezi kwa uzalendo wako uliouonyesha.

Anonymous said...

and has nothing to lose by naming them. Tutawajua na tuone serikali itafanya nini. Bila shaka ita puuza tu jambo hilo.

Anonymous said...

Mungu Akusamehe. na kwa kuwa umeshatubia basi nakuomba uendelee kutubia kwa Mungu na Mungu Atakusamehe na kwa kuwa umejua kosa lako basi Mungu Atatimiza uwezo Wake kwako. na Kwakuwa umejua kosa lako basi nakuomba usimfiche na wala usiogope kumtaja mtu yeyote unaemfahamu katika tatizo hili la madawa ya kulevya kwani mtegemee Mungu tu kukupa msadaa, je hao waliokutuma wanakupa msada gani kwa sasa? basi mtemee Mungu na tegemea kutoka kwake tu. na usiogope na wala usione aibu kumtaja hata kama mtu awe mkubwa kiasi gani kwani hakuna aliyemkwa katika hii dunia na huu ukubwa wanajipachika ndio sababu wanatuteketeza sisi wanyonge. aliye mkubwa kwa Mungu ni yule anaemuogopa Mungu zaidi na akawa na huruma na binadamu wenzake.

Anonymous said...

Asante kijana kwa ujasiri. Vigogo mnaimaliza roho ya mtu kwa madawa,mwogopeni Mungu. Hizo fedha chafu ndizo zinaibusha magorofa kama uyoga. Zamani madawa yaliingizwa sana na wafadhili wa timu kubwa Tanzania kama Simba, Yanga nk. Leo jeshi,polisi ndiyo vyombo vikuu vya kusaidia kuingiza. Wenzetu Kenya walishindwa kabisa sababu hizo ndizo kazi vigogo. Waziri wao wa mambo ya ndani alikufa na orodha ya majina ya vigogo kwenye helikota. Tunawakumbuka akina Kataballo kuhusu The Loliondo Gate,yuko wapi. Marehemu Sokoinne yuko wapi, G55 wako wapi, kijana chipukizi wa CCM(Amina Chifupa) yuko wapi????????? Wachangiaji kazi kwenu.