amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwamo kukutwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Sh. milioni 68.
Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.
Wakili wa serikali Leonard Challo alidai kuwa Agosti 4, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere alikamatwa na askari akiingiza kilo 1,512.69 za dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye thamani ya Sh. 68,069,250.
Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na tarehe ya tukio la kwanza mshtakiwa alikamatwa na askari akiingiza nchini dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 34.77 yenye thamani ya Sh.13, 908,000.

2 comments:
Oohhhh kilo 1,512.69 for only Tsh 68 million?
mnawaonea hawa wafanyabiashara wadogo wadogo kwa nini msiwakamate wafanya biashara wakubwa wanao leta unga kwa makontena tena wenye nyazifa zao serikalini na wanao wajua wana siasa acheni hizo duniani kama kweli mnataka kupiga vita unga basi wanafanya biashara hii ni watu wenye nyazifa zao na ndo maana hawaguswi wana guswa hawa wadogo wadogo inanitia kichefu chefu nikisoma habari hizi daima wakubwa hawakamwatwi wadogo wadogo ndo wanakomeshwa na kumomolewa wakubwa wanakaa na kucheka majumbani mwao na maaofisini pamoja na maswahiba zao
what a shame but thats how life is now days samaki mkubwa kummeza samaki mdogo what a shame tanzania
Post a Comment