Dk. Salim Ambaye pia ni Waziri Mkuu msataafu na Katibu Mkuu mstaafu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Baraza hilo, ambao ulihudhuriwa na Mabalozi wastaafu, wafanyakazi wa wizara hiyo pamoja na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.
Alisema kabla ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume hiyo na hata baada ya kuteuliwa, amekuwa akisafiri mara kwa mara na kukutana na Watanzania ambao wanaishi nje ya nchi na wengi wao wamekuwa wakizungumzia kuhusiana na suala la uraia, na wanalizungumzia zaidi suala la uraia wa nchi mbili, hivyo wizara hiyo inaweza kusaidia sana kwa kutoa mchango wake kutokana na uzoefu uliopo.
Aidha Dk Salim aliongeza kuwa wizara hiyo ina nafasi nzuri zaidi ya kuchambua na kushauri jinsi ya kutumia vizuri rasilimali za nchi kuendana na uzoefu walioupata kutokana na kufuatilia na kutembelea nchi nyingine duniani.
Akizungumzia suala la Muungano, alisema wizara hiyo ipo katika nafasi nzuri ya kuchangia katika suala la katiba gani inahitajika kwani moja ya dukuduku kubwa la Wazanzibari ni kwamba Muungano kwa ulivyo sasa hauwapi nafasi ya kutambulika, na kupata ushirikiano katika medani ya kimataifa hasa kwa yale mambo ambayo si ya Muungano.
“Muundo wa Muungano umekuwa ni jambo ambalo limejadiliwa sana na kuonyesha tofauti kubwa kwa wachangiaji mbalimbali, kutokana na uzoefu wenu wa mambo ya nchi za nje na mchango wenu kama wizara inayotetea maslahi ya Tanzania kwa ujumla, na uzoefu uliopatikana mpaka sasa mnaweza mkachangia vizuri pia katika suala la Muungano,” alisema.
CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Finally Somebody raised our voices. Sielewi kwa nini serikali yetu haiwezi kushirikiana na nchi za Afrika zilizoruhuru uraia wa nchi zaidi ya moja na kujua jinsi gani nchi hizo walihandle hii issue. Rais Kikwete ongea na rafiki jirani hapo Kenya uone ni jinsi gani Katiba yao inasema na sheria za uraia wa nchi mbili kwani wenzetu wapo juu sana kimaendeleo. Look at their currency!!!
Post a Comment