Kwenye post hii tunajiunga na bbcswahili.com ambao wameandika….. kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa mwisho wa sekondari na hiyo inamaanisha hakuna hata mmoja ambaye atafuzu kuingia chuo kikuu.
Waziri wa elimu wa Liberia anakwambia ameshindwa kufahamu ni kwa nini Wanafunzi hao zaidi ya elfu 25 wamefeli kwa kiasi hicho ambapo kwenye sentensi nyingine Wasimamizi wa chuo hicho wameiambia BBC kwamba hawa Wanafunzi hawakuwa makini na pia walikosa ufahamu mzuri wa lugha ya Kiingereza ambayo ndio ilitumika.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf amekiri kwamba mfumo wa elimu kwenye nchi yake bado ni duni na unahitaji marekebisho ya dharura ambapo hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa wanafunzi wote kufeli mtihani huo licha ya kulipa ada ya usajili ya dola ishirini na tano.
Chuo hicho kikuu cha Liberia ambacho kina idadi kubwa ya wanafunzi, hakitakuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakati muhula mpya mwezi ujao.
Baada ya matokeo kuonyesha kwamba wote wamefeli, Wanafunzi wengi wanasema hawajaamini matokeo ya mtihani huo ambapo pia waziri wa Elimu Etmonia David-Tarpeh ameiambia BBC, anatarajia kukutana na wasimamizi wa chuo hicho ili kujadili hiyo ishu.
No comments:
Post a Comment