ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 17, 2013

JOSE MOURINHO HAJUI VICTOR MOSES ALIPO

Mchezaji Victor Moses (13) akishangilia moja ya mabao yake kwenye timu ya Chelsea FC

Mchezaji wa kimataifa wa Nigeria anayekipiga timu ya Chelsea ya Uingereza, Victor Moses ameondolewa na Jose Mourinho kwenye kikosi cha Chelsea kitakachojitupa uwanjani kesho na Hull City kwenye ligi kuu ya ya nchi hiyo iliyoanza leo.

Victor Moses alikwenda kuchezea timu ya Nigeria kwenye wiki hii ambayo ilikua wiki ya mechi za kitaifa lakini hajarejea Uingereza na wala hajawasiliana na club yake.

Kocha Jose Mourinho amesema hawezi kumpanga David Luiz kwa sababu ni majeruhi, Victor Moses amesema amemuandoa kikosini kwa sababu hajui alipo vilevile mchezaji Azpilicueta huenda asicheze mechi ya kesho kutokana na kusafiri kwenda Ecuador kukaa bechi kwenye timu yake ya Taifa.

Kuhusu Victor Moses viongozi wa Chelsea wanasema alitakiwa mazoezini Ijumaa lakini hakutokea na wala hakuijulisha Club kwanini hakuhudhuria mazoezi kilichobakia ni kuhisi tu kwa viongozi hao kwamba huenda alikosa ndege ya kurudi Uingereza na wanatumaini hakuna jambo baya lililompata.

Victor Moses alikwenda kuichezea timu yake ya Taifa ya Nigeria ilipocheza na Afrika ya Kusini na kuibuka na ushindi wa bao 2-0 siku ya Jumatano kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa na mchezaji huyo aliingia kipindi cha pili badala ya Sunday Mbia.

Uwezekano ni mdogo kwamba Moses amefikwa na jambo kubwa lakini kwa yeye kutoka Nigeria chochote kinaweza kutokea, mwaka 2011 mchezaji mwingine toka Nigeria anayekipiga Chelsea John Obi Mikel ilibidi awe na wakati mgumu baba yake mzazi alipotekwa kwa siku 10.

Mwaka 2008 mchezaji mwingine na timu kepteni timu ya Taifa ya Nigeria, Joseph Yabo alijikuta kwenye wakati mgumu pale maharamia wa Nigeria walipomteka mdogo wake.

Hatutegemei chochote kibaya kimemtokea Moses tunatumaini kila kitu kitakua sawa.

No comments: