
Chimene Kpakanale ni mama wa miaka 22. Yeye ana bahati ya kujifungulia mwanawe wa kiume hospitalini, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati. Akina mama wenzake wamelazimika kuzalia wanao kambini au vichakani kufuatia mapigano nchini humo.

Bw. Nzu aliwasili eneo la Batalimo kutoka nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo alitoroka mapigano.Kwa sasa anaishi kwa nyumba hii ya matope akiwa na mkewe na wanawe wanne.

Bi Kpakanale alijifungua mwanawe wa kiume hapo Julai 17. Kabla ya kuondoka hospitalini alipokea chanjo dhidi ya kifua kikuu na kupooza.Mhudumu wa shirika la Merlin Jacob Zocherman amesema uhaba wa chanjo umepelekea kulipuka maradhi ya ukambi na tetekuwanga

Kwa wakati mmoja kituo hiki kilikumbwa na uhaba mkubwa wa dawa. Hali mbaya ya usalama ililazimisha magari ya kutoa misaada kuhifadhiwa katika nchi jirani ya DRC.
No comments:
Post a Comment