ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 21, 2013

MAMA WA BINTI KIZIWI AFUNGUKA KUHUSU KIFUNGO CHA MTOTO WAKE HONG KONG

Imelda Mtema na Denis Mtima
HATIMAYE mama mzazi wa Sandra Khan maarufu Binti Kiziwi, amefunguka kuhusu madai kwamba mwanaye amenyongwa nchini Hong Kong baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.

Mama huyo aitwaye Rehema Selemani mkazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar, amesema kuwa mwanaye amefungwa miaka mitatu na nusu na anawasiliana naye kwa njia ya simu kila baada ya miezi miwili.

“Taarifa za mwanangu kunyongwa si za kweli bali amefungwa miaka mitatu na nusu,” alisema mama huyo.
Mama huyo amemtupia lawama rafiki wa karibu wa Binti Kiziwi aliyemrubuni kufanya biashara hiyo ya kusafirisha madawa ya kulevya.

“Sikuijua safari hiyo ya mwanangu ila nilipigiwa simu na rafiki yake wakiwa wameshafika Nairobi, Kenya,” alisema.

Kama vile haitoshi, mama huyo anamlaumu rafiki kwa kuchukua dola 5,000 za mwanaye alizokutwanazo wakati akikamatwa.
Mbali na kuwasiliana na mwanaye, mama huyo amesema Binti Kiziwi amekuwa akimtumia fedha licha ya kwamba yuko gerezani.
“Ananitumia fedha, anasema kuwa huwa wanafanya kazi wakiwa gerezani na kulipwa,” alimalizia.

Source:Global Publishers

3 comments:

Anonymous said...

We bibi avuliwae nguo huchutama. Hivyo basi acha kulaumu watoto wa wenzako. Binti yako anaonyesha ni tamaa na kataka utajiri wa haraka nahayo ndio matunda yake. Usiwatupie wana wa watu lawama kwani mwanao hana udogo wa kushawishiwa.

Anonymous said...

Wewe mama shindwaaaa kabisaaaa, Mwanao Alitaka utahiriiii wa harakaaaa harakaaaa bila kutokana jasho sasa matokeo yake ndo hayoooo amejiingiza kweeenye matatizoo makubwa!!! Uroho na ulaku wa Mali ndo umemponzaaa! Na mtoto aliyelelewa kwa maadili mazuri na aliyefundishwa kumtukuza Mungu haweziiii kujiingiZa kwenye matatizoo! Kilichobakii wewe mama wa binti kiziwi muuombee tu atoke jela salama na awe na moyo wa kumpenda na kumuheshimu Mungu!