Tunapenda kutumia fursa hii kuwajulisha
juu ya kamati maalum ya muda – Kamati ya Mapendekezo ya Katiba ya Tanzania
(KAMKATA).
Lengo la kamati
hii ni kuhakikisha kwamba kila Mtanzania aishie Marekani anapata fursa ya
kushiriki kikamilifu katika jambo la kihistoria la kutoa maoni na
mapendekezo kuhusu Rasimu
ya Katiba iliotolewa na Tume
ya Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo
June 3, 2013.
Kamati hii
imeundwa kwa ushirikiano wa baadhi ya wanajumuia na viongozi kadhaa wa jamii za
Watanzania waishio hapa nchini.
KAMKATA ni
chombo cha kujitolea, kinachofanya kazi zake kwa kufuata utaratibu uliotolewa
na Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba –
Mheshimiwa Jaji Mstaafu Joseph Warioba. Unaweza kutembelea tovuti ya Tume
Taifa ya Marekebisho ya Katiba taifa kwa kujionea shughuli mbali mbali na hatua
mbalimbali zilikokwishafanywa na zinazoendelea kufanywa na Tume hii ya Taifa.
Vilevile kwenye tovuti hiyo unaweza kupata Rasimu ya kwanza ya Katiba mpya
ambayo ndio inatolewa maoni sasa hivi www.katiba.go.tz
KAMKATA
inatarajia kuendendesh shughuli zake kwa kushirikiana na ofisi ya ubalozi wa Tanzania hapa
Marekani na makundi mbalimbali ya Jumuia za Watanzania hapa nchini.
Viongozi wa kamati hii ni:
Nassor Ally – Katibu
Anthony Tinru - Mjumbe
Kadari Lincoln Singo – Mjumbe
Erick Byorwango – Mjumbe
Rabia Dahal – Mjumbe
Njia tutakazozitumia katika kuwasiliana na wanajamii ni
pamoja na kupitia kwenye Jumuia za Watanzania, vyombo vya matangazo, tovuti ya
kamati, (iko kwenye matengenezo ya mwisho) barua pepe katibatz@yahoo.com , na kwa njia za simu (415)316-5247
Kikomo cha zoezi hili ni August 25, 2013.
Utakapopata
taarifa hizi, unaweza kuanza mawasiliano na kamati hii na kuleta maoni yako kwa
kutumia njia ya mawasiliano iliyopo hapo juu. Vilevile tunashauri
kuwafahamisha wengine na kupeleka ujumbe huu kwenye uongozi au jamii yako.
Tunategemea kila
mmoja wetu atakua pamoja na kamati hii na kutoa ushiriki mpana kwa kuchangia na
kutoa mawazo yake kwa uhuru na uwazi.
Uwezekano wa zoezi hili utatokana na ushirikiano wetu sote.
Tunashukuru sana .
KAMATI YA RASIMU YA KATIBA (KAMKATA) MAREKANI.
Erick Byorwango
