Advertisements

Monday, August 12, 2013

MASTAA BONGO MVUTO WAO SIYO WA KUMULIKA NA TOCHI!

Je, mvuto, urembo na uzuri ni vitu gani? Ni kweli kwamba uzuri au urembo uko katika mboni ya jicho la mtazamaji au kwenye akili na macho ya binadamu? Ukweli ni kwamba kila mtu ana namna yake ya kutafsiri maneno hayo.Wema Sepetu.
Staa wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade huwa anamshukuru Mungu kila kukicha kwa kumuumba mzuri na mwenye mvuto. Je, wewe unafanya hivyo?

Katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo kuna mambo mengi ambayo ukurasa huu kama kawaida yake huyatazama na kukuletea wewe msomaji.

Bongo kuna mastaa wengi wa
Nancy Abraham SUMARI


Huyu ni Miss Tanzania na Miss World Africa wa mwaka 2005. Kilichomfanya akatwaa mataji hayo ni mvuto na uzuri alionao ambao hakika Mungu amempendelea. Kwa mwanaume kamili, ukipishana naye huna jinsi ya kukwepesha macho kumtazama. Kuna taarifa kuwa kwa sasa ni mke wa jamaa anayetajwa kwa jina moja la Luca.

Faraja Kota NYALANDU
Ni Miss Tanzania wa mwaka 2004 ambaye alishinda taji hilo kutokana na mvuto aliokuwanao ambao ameendelea ‘kuumeinteini’ hadi leo. Anapaswa kumshukuru Mungu kwa kumuumba ‘kichuna’. Kumbuka kwa sasa ni mke wa ndoa wa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) na Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii, Lazaro Nyalandu. 

Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-LYINN’
Huyu ni Miss Tanzania wa mwaka 2000 na pia mwanamuziki wa Bongo Fleva lakini siku hizi hasikiki. Mvuto na uzuri aliokuwanao bado anao ndiyo uliomfanya kushinda ‘krauni’ hiyo. 
Jokate MWEGELO
Ni Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006. Ana ‘taito’ nyingi kama mwigizaji, MC, mtangazaji, mwanamitindo, mwanamuziki na mjasiriamali anayemiliki lebo ya mavazi ya Kidoti. Ni mzuri na ana mvuto wa aina yake unaowanyima wanaume wengi usingizi. Bado hajaolewa.

Hoyce TEMU
Huyu ni Miss Tanzania wa mwaka 1999 ambaye kwa sasa ni Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa kwa hapa Bongo. Ni mwandishi wa Kitabu cha Nayakubali Yote. Anajishughulisha na kusaidia jamii kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kupitia Runinga ya Chanel Ten. Pamoja na kuwa mke wa mtu na mtoto mmoja, bado mvuto wake upo palepale. 

Lisa JENSEN
Huyu ni Miss World Tanzania wa mwaka 2012 ambaye pia ni mwigizaji wa filamu za Kibongo. Ukimuona Lisa lazima utakiri kuwa Mungu kamuumba na kweli kaumbika. Bado hajaolewa lakini kwa sasa ana ‘kibendi’.

Wema Isaac SEPETU
Ni Miss Tanzania wa 2006 na mwigizaji wa filamu za Kibongo ambaye anatarajia kuanzisha kipindi chake cha In My Shoes kupitia Clouds TV. Anajiita Beautiful Onyinye akijilinganisha na mrembo anayesifiwa katika wimbo huo ulioimbwa na P-Square kutokana na mvuto wake japo kwa sasa analalamikiwa kujiharibu kwa kujichubua. 

Millen MAGESE
Millen au Happiness Magese ni Miss Tanzania wa 2001 ambaye pia ni modo wa kimataifa. Kwa sasa ana makazi nchini Marekani. Bado ukimuona mtoto ‘anaita’ kutokana na mvuto alionao kiasi cha kupamba majarida mbalimbali makubwa nje ya Bongo.

Salha ISRAEL
Huyu ni Miss Tanzania wa mwaka 2011 ambaye hivi karibuni alizama kwenye filamu za Kibongo. Mrembo huyu ana mvuto kiasi kwamba akikatiza lazima wanaume wageuke kukamilisha fahari ya macho.

Vanessa MDEE
Van Vee au Van Money ni Mtangazaji wa Radio Choice FM ya jijini Dar. Pia ni mwanamuziki, alisikika vema kwenye ngoma kama Me and You na Closer. Ni balozi wa vijana Tanzania na hajaolewa. Kuhusu mvuto, Vanessa ni ‘chuma’.

No comments: