ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 17, 2013

MENO YA TEMBO YAKAMATWA UWANJA WA NDEGE DAR

Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dares Salaam, ndugu Katto akionesha meno ya Tembo yaliyokamatwa yakiwa yametengenezwa mithili ya bangili tayari kwa kusafirishwa.
Kamanda Katto akionesha meno ya tembo yaliyotengenezwa kama vijiti.
Jana Agost 16 mwaka huu majira ya saa 10:46 jiono polisi jijini Dar walimkamata raia wa Vietnam aitwaye Nguyen Fanichati akiwa na meno ya Tembo, Tukio hili lilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Meno hayo yaliyokuwa yamefichwa ndani ya sanduku yalitajwa kwa ujumla kuwa na zinathamani ya Tsh. milioni 18.4

2 comments:

Anonymous said...

Mimi nafikiri hata serikali inatakiwa kuona aibu na kulifungia kazi swala hili la madawa ya kulevya mara pembe na hiyo tindikali!! Wahusika wako hapa hapa Tanzania, Kariakoo kuna biashara chungu nzima hazina hata mapato lakini utakuta mtu anafungua tangu asubuhi kufunga jioni. Hatujiulizi tu kuna nini? Waliokamatwa kuhusika na madawa si wana anwani wanakoishi na wadhamini ni lazima hayo maeneo yafuatiliwe ipasavyo. Hili sio swala la kusema uwanjani tu! waangaliwe hadi wanakotoka watapata hata marafiki wao wanajua mtandao mzima. Tanzania inaoza tukiangalia hivi hivi, viongozi mpo wapi.??

Anonymous said...

WIZI MTUPU