Waheshimiwa wakikaribishana kwenye meza kuu kwenye sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika 30 Overhill Rd Mt Vernon NY. Sherehe iliandaliwa na Waislam wa New York na kuhudhuriwa na wanajumuiya wote pamoja na familia zao bila kujari imani za dini zao. Hiyo ndiyo dhana tunayojivunia Watanzania ya kushirikiana katika shughuli za kijamii bila kubaguana Tanzania Oyeeee Mungu ibariki Tanzania.
Katibu wa jumuiya ya Watanzania New York bwana Shaban Mseba akiongozana na Mgeni rasmi Mh. Balozi Manongi muda tu alipowasili kwenye sherehe hiyo.
Mh. Balozi Manongi akiongea machache mbele ya watanzania waliojumuika pamoja na familia zao kwenye sherehe hiyo.
Sherehe Eid El Fitr iliudhuriwa na mabalozi wetu wote wawili wa hapa New York, Hapa ni Mh. Balozi Mwinyi akiongea kwenye sherehe hiyo.
Hapa ni Mh. Balozi Mero akiongea machache na pia alitumia nafasi hii kuwaaga wanaNew york, Mh. Mero ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania mji wa Geneva nchini Switzerland na muda wowote ataodoka kuelekea huko..
Katibu wa new York Community bwana Shaban Mseba akiongea machache.
Bwana Hajji Khamis mwenyekiti wa New York Community akitoa chukrani mbele ya watanzania waliojitokeza katika sherehe hizo za Eid El Fitr.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Baada ya hivi karibuni kurudi toka safari ya Dubai na Saudia Shekh Maftah alipata fursa ya kutoa mawaidha.
Juu na chini ni Shekh Maftah akiongoza Dua kwenye sherehe hiyo
Mjasiriamali David Mosha akiongea machache baada ya kupata nafasi ya kuongea kama kijana mwenye maendeleo. Akitoa ujumbe kwa vijana hasa changamoto za maendeleo zinazo patikana Tanzania. David Mosha alikuwa Marekani kwa likizo na aliongea na Watanzania sehemu mbali mbali alizotembelea.
David Mosha akisalimiana na waheshimiwa Mabalozi..
Dr....Temba akisalimiana na Mh. Balozi Manongi
8 comments:
ILIKUA MARA YA KWANZA WATANZANIA NEW YORK WANASHEHEREKEA EID EL FITRI. MUNGU WABARIKA WATANZANIA NA IBARIKI TANZANIA. KWA MUJIBU WA HABARI DUA ILIOSOMWA NI KUBWA SANA NA INAWAUNGANISHA WATANZANIA HATA WALE WALIOKUA NA TOFAUTI HAPO AWALI. ASANTE SHEIKH MAFTAH
tukiweka comment zetu luka unazibainia so its okay nachowabia hawa jamaa wamefanya jambo jema na zuri kuona katika state yetu tuna sherehekea eid na sisi kama watu wa dc lakini jamani nacho ona sisi jambo la dini si mchezo kila mtu anayo yake na siku yake ya kusherehekea japo kuwa sisi watanzania ni wamoja jamani tumuogope mungu
i hope utaweka comment yangu hii other wise dj luke yote kheir
hongereni sana watanzania wa new york kwa kufanya sherehe hii adhimu nakushukuruni sana tena sana kwa sababu na sisi sasa tutapoa moto kuruka kila leo dc lakini kitu kidogo tu jamani sherehe ya eid huwa inasherehekewa na akina nani?
watanzania ni wamoja na tumechanganya damu na wenzetu lakini jamani sherehe ya eid inasherehekewa na nani seriously naomba kujibiwa ahsanteni
dua hazipandi bwana msijidanganye ndo maana sijakuja huko kwa sababu sherehe ya eid ni ya waislamu na si ya mchanganyiko call me what you want but thats the fact tunawapenda ndugu zetu wasio waislamu lakini jamani chonde chonde kwa skukuu kila mtu anayakwake labda 4 of july nyama choma ndo mchanganyo kwa wote. ramadhan mbona hatufungi wote
baa ustadh hajj nakuona baaa unatoa dua ya nguvyu hongera maalim wetu , maalim sheikh na dj bilal mbona hampo kwenye dua
Alianza kwa kusema inapotolewa salam, basi ubaya na maovu yaliokua miongoni mwa jamii hufukiwa na mazuri na wema hutawala. Hiyo ndio maana ya salam. "Alinena Sheikh Maftah wa New York". Skeikh huyu hukubalika anapotoa nasaha kwa umma wa watanzania na hata jamii kutoka sehemu nyingine, basi hukubalika.Tunakubali kwa dhati kwamba umoja ni nguvu. Alirejea sheikh huyo na kukumbusha wimbo wa Taifa la Tanzania. Alidai kuwa watanzania wote ni wamoja na umoja huo haukuanza juzi ao jana kwani Mungu ibariki Tanzania ni wimbo wa amani. Hamid
naona watanzania mnanichafua!! sherehe ya eid ni ushindi wa kukamilisha nguzo moja kati ya nguzo tano za kiislam. ambapo muislamu wa kweli NILAZIMA asimame nazo!! kama umerehemewa akili timamu, afya njema,na uwezo halali wa mali basi ni lazima utekeleze nguzo 5 za dini inayohusia na sherehe ya eid ambayo inambata na sadaka na zakka.. na
Uislamu unahimizaa imani na ihsani kwa ndugu,jamaa,jirani,na marafiki na hata mpita njia.sherehe ya eid baada ya ushindi wa mfungo wako Wa R'dhani ni kuisherekea na wahusika niliokutajia hapo juu.usime ukrito au uisilamu. shereheka ushindi wako wa nguzo yako kwa IMANI NA IHSANI NA JAMII YAKOOO.ACHENI IZO!!! MTAKOSEANA UBINADAMU AMANI NA UPENDO DINI ZETU WATANZANIA
LOH MNANICHAFUA..
Nyinyi mnataka kuleta tofauti katika jamii, sherehe gani utaifanya peke yako au wewe na familia yako tuu??
Mfano mzuri viongozi wetu walialikana kwenye Idd na kusherhekea pamoja, sasa utasema hata kula mezani ni kosa na pia kutumia vijiko kosa, kukaa kwenye kiti kosa, kutovaa kanzu kosa, sherehe bila pilau, biriani kosa.
Dunia imebadilika wewe kama imani yako iko imara hakuna neno shirikiana na bindamu wenzajko mambo ya ukafri acha, la sivyo ukiendelea hivyo utaitwa AL QUEDA.
Post a Comment