Advertisements

Wednesday, August 14, 2013

Polisi wamkamata aliyemuua Msuya- Mwananchi

Arusha. Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na makachero.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.
“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha za kununua pikipiki na siku moja kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.
Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.
Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio zikahifadhiwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.
Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni mazuri.
lakini hakitatajwa jina lake.

4 comments:

Anonymous said...

vizuri sana jamani , mimi binafsi haya mauji yamenisikitisha sana

Unknown said...

Mbona hawataji jina lake au bado ni mtuhumiwa si mhalifu

Anonymous said...

Kama kweeli Police wamemkamata aliyesababisha mauaji hayooooo ya ki Nyama tena Kigaidi itakuwa vey a sana! Hata Kama alikuwa mbaya kiasi gaani haiku na anayestahili Kufa kifo cha kinyama hivyoooooo! Na pia aliyefanya hivyoooooo ametishia Amani ya Arusha kabisaaaa!!!! Jamani apatikaneee na hakumiwe KIFO tu iLi iwefundishooo kwa vibaka woote.

Anonymous said...

Kama kweeli Police wamemkamata aliyesababisha mauaji hayooooo ya ki Nyama tena Kigaidi itakuwa vizuri Sana!Hata Kama alikuwa mbaya kiasi gaani hakuna anayestahili Kufa kifo cha kinyama hivyoooooo! Na pia aliyefanya hivyoooooo ametishia Amani ya Arusha kabisaaaa!!!! Jamani apatikaneee na ahukumiwe KIFO tu iLi iwefundishooo kwa vibaka woote.