Advertisements

Wednesday, August 28, 2013

SHOGA, ASUBUHI MPE MUMEO KIAMSHIO, NI MUHIMU SANA

Shosti wangu, nakukaribisha kwa mara nyingine kwenye safu yetu hii. Shoga yangu somo la leo linataka utulivu kidogo unielewe na likikukaa kichwani, basi ndoa yako itakuwa salama miaka 100.

Hutakiwi kujisahau mama, mwanaume wako atakwenda nje, shauri yako! Mwanaume aliyekamilika lazima aamshwe asubuhi. Tena siyo kwa kurukaruka, la hasha! Mwamshe kwa utulivu, umfanye aamke akiwa mwepesi.
Mwanaume anapoamshwa asubuhi, inamwondolea uchovu, hata akili inachangamka, hapo anakuwa kamili bin tayari kwa ajili ya ujenzi wa taifa. Shoga, mpaka sasa hujaelewa mwanaume anaamshwaje? Unajua sana, hebu nitolee umbeya huko!
Hii inawahusu sana wale wanawake ambao wanatabia ya kuamkia kwenye majungu ya vitumbua, maandazi ukiuliza eti ni biashara. Hivi mwanaume akitoka nje ya ndoa kwenda kutafuta kuamshwa utaweza kufanya biashara zako na zikaenda kweli?
Mwingine anadai anafanya usafi wa nyumba. Acha mambo hayo wewe. Jitulize hapohapo kitandani, mvutie baba watoto kwa mambo matamu, baada ya hapo hakikisha unampa kiamshio ili aamke.
Unaposhindwa kumuamsha mumeo asubuhi, unamwacha kwenye bahari yenye kina kirefu na unampa nafasi ya kuwa mzito katika kila jambo. Kwa nini usimsaidie mwezako? Unataka huduma hiyo apewe na nani?
Mwingine anaamka amechoka ati! Hebu acha mambo yako, kilichokuchosha nini. Aliyekwambia nani kama kiamshio cha asubuhi kinaongeza uchovu?

MWANAUME ANAAMSHWAJE?
Ikifika alfajiri mwanamke kuwa wa kwanza kuamka kitandani, baada ya hapo fanya uchokozi wako kwa kumwamsha taratibu. Tena huo ndiyo muda wako wa kutumia utaalamu wako wote kuhakikisha anakuwa tayari kwa kupokea kiamshio kutoka kwako.
Endapo atapata kiamshio na umempa inavyotakiwa, utakuwa umefanikiwa kumfanya aamke akiwa amechangamka sawia na mawazo yake yote yatakuwa kwenye kazi.
Baada ya hapo, mpeleke bafuni akaoge, akitoka huko akute umeshamwandalia kifungua kinywa kizuri. Hakikisha kina mvuto ambacho anakipenda. Huo ni ushindi shoga.
Atakapotoka kwenda kazini, mawazo yake yote hujikita nyumbani. Aende nje kutafuta nini ikiwa raha zote anakutana nazo nyumbani? Shoga yangu, wengi wanasalitiwa kwa sababu ya kujisahau.

KWA WAVIVU
Kwa wale mnaoendekeza kazi za ofisini kama kigezo cha kuchoka, huo ni uvivu, itakula kwenu. Eti unaamka alfajiri unawahi kazini je mumeo akitoka nje na kwenda kutafuta huduma mbalimbali utaweza kufanya hizo kazi kweli au ndiyo utalia na kusema umerogwa na vimada usipendwe?
Wanawake wenzangu tuache visingizio kama wewe unafanya kazi kumbuka mume ndiyo kitu cha kwanza kwani umewaacha hata wazazi wako kwa ajili yake, kwa nini usimtimizie haki zake kwa kufuata mienendo iliyo sahihi? Kama una kazi za mbali au muhimu na yeye muweke kwenye ratiba ili usiharibikiwe upande mmoja.
Mume hapatikani popote bibi, si rahisi kihivyo. Kazi zinatafutwa hata kwa kuhonga na utapata, lakini ndoa utamuhonga nani? Je, utafanya nini ili kumpata yuleyule uliyefunga naye ndoa? Badilikeni mashosti ili kujenga nyumba ikae salama.
Mwisho nikukumbushe kuwa karibu na mumeo usiku wote. Mnapokaa sebuleni, talii kiwiliwili chake kama mpiga gitaa, hapo utamsababishia kukitamani kitanda, hivyo kulala mapema. Mkiwa kitandani mapema, itawarahisishia kufanya shughuli zenu mapema ili asubuhi mkiamka, muendelee na kazi za ujenzi wa taifa.

GPL

2 comments:

Anonymous said...

Mapenzi hayana fomula, ila ni bahati upate mtu unayempenda na yeye akakupenda. Thats it, dada zangu wala msihangaike wewe nenda zako kazini

Anonymous said...

uliyosema mdau hapo juu nakubaliana nawewe na nakupa kumi kweli mapenzi hayana formula sijui ufanya hivi na vile na vile na hivi kuna wanaofanyiwa yote hayooo yaliyoandikwa kwenye hii habari lakini mwamme kama kichaa anatoka na ma baby kibao tena wengine wake za watu so mambo ya zuga zuga tuyaache mtu akikupenda na wewe ndo unampenda basi ngoma itakuwa poa na pia kuheshimiana na kumuogopa muumba wenuu.
lakini pia nakubaliana na yaliyoandikwa kuna wanawake wengine wanakiburi sana hata kumtunza mume hawajui au sijui wanajiona jamaa kanifia mimi kila nikimwambia langu analifanyia hawajui jamaa anataka ndoa idumu tu siku akichoka basi anaweza kukubwaga mwana mama wee usiwe mvivu na utundu wako kwenye vijimambo na umuheshimu mumeo na kupenda na kutendea haki na umsaadiye sio ukipata pesa yako unaibana kuna siku atachoka na wako mwengi mitaani

narudia tena na kuumuunga mkono mdau wa mwanzo mapenzi hayana formula,muwe na upendo wa kweli wa dhati na kuoneana huruma na kujaliana siyo wewe unamfanya mwenzio chuma ulete hata chumzi inakushindwa kununua kisa mume ataleta akimpata wa njee kuna siku utajuta. jimwage mwana mama jimwage mpe mapenzi na yeye akupe mapenzi other wise jikateni kivyenu kama hakuna mapenzi