
Nyuma ya kioo: Luis Suarez, akiondoka mazoezini Jumanne, ameachwa kwenye kikosi cha Liverpool kinachokwenda Norway

Suarez atakwenda kufanyiwa vipimo ili kujua uzito wa maumivu yake kama ataweza kusafiri kwenda Dublin Ijumaa kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Liverpool wa kujipima dhidi ya Celtic Uwanja wa Aviva.
Tangu amerejea kutoka mapumziko yake ya majira haya joto, Suarez amecheza akitokea benchi katika mechi dhidi ya Melbourne Victory, Thailand na Olympiakos Jumamosi iliyopita, huku akizungumziwa sana kuondoka Anfield.

Hana furaha: Suarez anatarajiwa kuondoka Liverpool, na Arsenal iko mstari wa mbeke kumsajili

Benchi: Brendan Rodgers anakwenda na timu yake Oslo kumenyana na Valarenga bila Suarez
Liverpool imeendelea na msimamo wake wa kutotaka kumuuza Suarez, ingawa anahusishwa kwa kiasi kikubwa na Arsenal.
Timu ya Arsene Wenger imekwishatoa ofa mbili - moja ya Pauni Milioni 35, nyingine ya Pauni 40,000,001 - ambazo zote zimepigwa chini.
Kukosekana kwake kesho hakutavuruga mipango ya Rodgers kuelekea msimu mpya, kwani Suarez atakosa mechi sita, akitumia adhabu yake iliyosalia kutokana na kumng'ata Branislav Ivanovic.
Rodgers amemchukua pia Daniel Sturridge aliyerejea baada ya kupona kifundo cha mguu.

Tegemeo: Itakuwa pigo kubwa kwa Liverpool ikiwa Suarez ataondoka

Kocha wake mpya? Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekwishatoa ofa mbili zilizopigwa chini Liverpool
No comments:
Post a Comment