
Mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite ambaye pia ni mmiliki wa hotel ya kitali ya S.G Resort ya jijini arusha Erasto Msuya amefariki dunia leo majira ya alasiri wakati alipokuwa akitokea porini kuelekea mjini. Kwa mujibu wa taarifa ambazo vijimambo zimezipata mara baada ya tukio hilo zinasema kuwa mfanyabiashara huyo alipigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi mara baada ya majibizano ya risasi yaliyotokea maeneo ya barabara ya kia. Kwa habari zaidi endelea kufuatilia Vijimambo tutaendelea kuwajuza nini kinaendelea HABARI KUTOKA LIBENEKE LA KASKAZINI BLOG
No comments:
Post a Comment