Pamoja na kumuwezesha mtu anayesafiri ndani ya Tanzania
kulipia huduma za malazi katika hoteli 142 zilizopo katika Mikoa mbalimbali
nchini Tanzania kwa njia ya mtandao, Vinjari (www.vinjari.co.tz) imeanzisha
huduma mpya ya kununua tiketi za ndege mtandaoni.
Kwa kushirikiana na kampuni ya Coastal Aviation, sasa mtu
yeyote anayetarajia kusafiri kwa njia ya ndege, anaweza kulipia tiketi yake kwenda
katika Mikoa mbalimbali Nchini Tanzania pamoja na Nchi za jirani za Uganda,
Rwanda na Msumbiji kwa kupitia Vinjari.
Huduma za malipo zinafanyika kwa kupitia Mpesa, Tigo Pesa,
pamoja na kadi za Benki za Visa na MasterCard. Tembelea https://vinjari.co.tz/v.php?listing=coastal
kwa maelezo zaidi.

No comments:
Post a Comment