ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 21, 2013

Warundi Simba wamwaga ahadi

Dar es Salaam. Wachezaji wa kimataifa wa Simba kutoka Burundi, Amis Tambwe na Gilbert Kaze wametua nchini juzi usiku na kumwaga ahadi  zisizo na idadi.
Wanandinga hao wamechelewa kujiunga na wenzao Dar es Salaam baada ya  kuzuiwa na klabu yao ya Vital ‘O’ ya Burundi.
Kaze, beki wa kati na tegemeo wa timu ya Taifa ya Burundi, aliliambia  gazeti hili kuwa amekuja kucheza soka Simba ili kuipa mafanikio.
“Simba waliniamini kunisajili, na mimi nimekuja kuwaonyesha hawakukosea kunisajili.
“Tatizo la beki wa kati halitakuwapo tena Simba. Nimekuja kuwafurahishwa Simba,” alisema Kaze ambaye akiwa na timu ya Taifa ya  Burundi anacheza beki ya kati na Hassan Hakizimana wa Atratical ya nchini humo.
Anaungana na beki Joseph Owino kutoka Uganda, wakisaidiwa na wazawa chipukizi, Adam Miraji, Rahim Juma, Hassan Khatib na Rajab Isiaka katika safu ya ulinzi.
Kwa upande wa Tambwe alisema: “Watanzania wanaopenda soka siyo wageni nami, ahadi yangu ni kuifungia mabao klabu ya Simba tu hadi kieleweke.”
Kwa upande wake Kocha Abadllah Kibadeni alisema kuwasajili kwa wachezaji hao kutaifanya timu yake kuwa imara. Tambwe na Kaze wamesajiliwa Simba, lakini mikataba yao ilikuwa imalizike baada ya ligi ya Burundi kumalizika.

No comments: