Mhe. Balozi Steven Matenje wa Malawi akiwa na Mhe. Palan Mulonda,Balozi wa Zambia nchini Marekani,(kulia) na Mhe. Martin Andjaba, Balozi wa Namibia nchini Marekani (kushoto)na Bw.Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC katika hafla ya uzinduzi wa Malawi Washington Foundation iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mhe. Balozi Steve Matenje,Balozi wa Malawi nchini Marekani akimkaribisha Bw. Suleiman Saleh nyumbani kwake Potomac,Maryland katika hafla ya uzinduzi wa Malawi Washington Foundation mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mhe.Steve Matenje,Balozi wa Malawi nchini Marekani amesisitiza kwamba Tanzania na Malawi ni nchi ndugu na zenye historia kubwa baina ya wananchi wake na kubainisha kwamba tofauti katika suala la mpaka katika Ziwa Nyasa litamalizika si muda mrefu. Balozi Matenje aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Washington Malawi Foundation iliyofanyika nyumbani kwake Potomac, Maryland. Balozi alimweleza hayo Bw. Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC ambaye alimwakilisha Mhe.Balozi Liberata Mulamula katika uzinduzi huo.. Balozi Matenje aliendelea kusema kwamba anaamini udugu uliopo baina ya wananchi wa Malawi na Tanzania ndio unaompa imani kubwa kwamba suala la mpaka litapatiwa uvumbuzi wa kudumu na kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.


No comments:
Post a Comment