ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 21, 2013

kuaga na kumkaribisha mwambata wa kijeshi mpya.


Brigedia Jenerali E. Maganga           Kanali Adolph Mutta

Unamkumbuka Brigadier General Maganga, yule Mwambata Jeshi aliyeagwa miezi
michache iliyopita na wanajumuia wa DMV, kwa shangwe, kwani alikuwa
amemaliza muda wake wa utumishi ubalozini Washington. Lakin kwa maagizo ya
ngazi zake za juu alirejea tena kuendelea na kazi huku akisubiri kuwasili
kwa Mwambata mpya. Wiki hii Mwambata mpya Colonel Adolph Mutta amewasili
rasmi na anatarajiwa kuanza kazi karibuni.
Safari ya jenerali Maganga kurejea nyumbani sasa imeiva. Na kutokana na
upendo wenu wana DMV kwake na familia yake anapenda kuwaalika kwenye hafla
fupi ya 'nyama choma' ya kuwaaga na kumkaribisha Mwambata Mpya,
itakayofanyika jumamosi( tarehe 21 September) kuanzia saa tisa mchana hadi
saa kumi na mbili jioni. Anuani ni 16608 Medinah Court, Silver Spring. MD
20905. Ukisoma taarifa hii mwambie na mwenzio.

3 comments:

Anonymous said...

Mungu awabariki na kuwapeleka nyumbani salama! Kusema kweli Baba General na Mama General hatutowasahau. You have been so close to the community, mmetuchekesha na kutufurahisha wakati wote. Tumeshirikiana katika misiba na sherehe na tunategemea mofisa wengine wa ubalozi wataiga mfano wenu. Maofisa wa Ubalozi wanatakiwa wajitahidi kuwa karibu na Jumuiya, shughuli zote za kijumuiya you were always there! Mungu akusafirishe salama na tungependa kuwa na namba zenu za simu au email you never know tukijaaliwa kuja bongo angalau tuwaone na tuendelee kuwasiliana.
We love you and we will truly miss your nice hotuba's!

Anonymous said...

Mzee maganga ndo anachia Jumba la serikali.... Mhh jitaidi watoto wasipate shida hapa USA maana maisha bila elimu ni bure... Ni ushauri tuu:

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe kabisa. Baba na mama wamekuwa wakiudhulia matukio mbalimbali bila tatizo. Tunahitaji watu kama hawa ktk community yetu. Mungu awatangulie na azidi kuwaongezea. Asanteni sana.