ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 4, 2013

Mama mwingine akamatwa na Madawa JNIA

Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam leo.


Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio zima la kunaswa kwa mtuhumiwa huyo ambapo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wakati kete hizo zimepelekwa kwa ofisi ya Mkemia Mkuu kwa uchunguzi zaidi. 




Anthonia Ojo akiwasili kituo cha polisi cha JNIA baada ya kukamatwa
Anthonia Ojo akielekea kupanda gari kuelekea kituo cha polisi.
Anthonia Ojo akiwa chini ya ulinzi.
Hati yake ya kusafiria
Begi lilibebewa madawa
Juu na chini ni Anthonia Ojo akitoa madawa alikokua amyaficha kwenye mikebe ya poda na shampuu
Kete alizokamata nazo
Anthonia Ojo akiwa kituo cha Polisi.
Madawa yakirudishwa kwenye mikebe baada ya kuonyeshwa kwa wanahabari.
Recodi ya Anthonia Ojo aliwahi kuja tena Tanzania mwaka 22011
Mama mmoja wa kinigeria amekamatwa na madawa ya kulevya mchana huu katika uwanja wa ndege wa JNIA akijaribu "kum-bypass " Dr.Mwakyembe.

Mwana mama huyo aliyetambuliwa kwa jina la Ojo Athnonie alikuwa amevaa bai bui kwa juu na kufunika sura yake yote.....
Taarifa zinaarifu kwamba mama huyo alikuwa akisafiri na na Ethiopian Airways kwenda Roma, Italy kupitia Paris na hivi sasa yuko chini ya ulinzi mkali wa polisi .....

Kaimu kamanda wa polisi katika uwanja huo, Kamanda Renatus Chalia amesema raia huyo aliingia nchini tangu tarehe 30 mwezi wa nane mwaka huu kama mfanyabiashara wa viatu na mikoba.

Anthonia Ojo (25) anadaiwa kutumia ubunifu wa ziada kwa kanunua powder za johnson kubwa na kuzikata kwa juu
na kuweka kete 99 za madawa ya kulevya ndani ya mikebe hiyo.
Chanzo: Robert Okanda

3 comments:

Anonymous said...

Baibui kubwaaaa, unaharibu maana ya ushungi, umevaa hivyo ili watu wakuamini?kumbe ni bedui mkubwa, alaaaaah.Mwizi mkubwa.

Anonymous said...

wee mdau wa mwanzo kuwa na heshima si vizuri kumtukana mwanamama wa watu kwani hujawaona masister nao wakifanya vitoko vyao kanisani na sehemu zinginewe au unadhani hatuyajui

Anonymous said...

mwakyembe naye si msafi kama mkikumbuka wadanganyika kama mnakubukumbu ya historia yenu basi mwakiyembe mbona ile ripoti ya bajeti alifeka kimya kimya hajajieleza eti reo amekuwa masihii wa kuwakamata watu wanaoleta madawa yakulevya wakati serikali ya tanzania toka utawala wa juu mpaka wa chini umeoza kwa madawa ya kulevya unadhani hatujui acheni hizo

mwachiyeni mwanamke wa watu chap chap na umeona jina si muislamu ila anataka kukashifu dini lakini mungu kawaona