ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 4, 2013

Maneno ya Serikali ya Tanzania kuhusu ushuru ulioongezwa kwa malori ya Tanzania yanayoingia Rwanda


Serikali ya Tanzania imekiri kujitokeza kwa tatizo la kuzuiliwa kwa maroli ya mizigo katika mpaka wa Lusungu, malori yatokayo Tanzania kuelekea Rwanda.
Ilikua ni ishu nzito ambayo pia imemiliki headlines kwa kipindi hiki kifupi lakini sasa Serikali inakwambia tatizo limeshughulikiwa na tayari mizigo imeanza kupitishwa.
Namkariri Waziri Tizeba akisema ‘tulichukua hatua mara moja kutafuta viongozi wahusika wa Rwanda kujua hicho ni kitu gani ambapo Waziri wa fedha wa Rwanda alikua ametoa agizo hilo kwa mdomo kwa mamlaka za forodha Rusumo waanze kutoza hiyo tozo kwa magari yenye usajili wa Tanzania, baada ya kuzungumza nae waziri Rwakabamba walifanya mazungumzo na wenzake na ndani ya nusu saa jambo hilo likazuiliwa kuendelea kufanyika pale mpakani na magari yetu yakapita kwa kulipia viwango vya zamani, tutaendelea kulishughulikia hili jambo kwa haraka zaidi’
Hii ni kauli ya naibu waziri wa Uchukuzi Dr. Charles Tizeba anaekwambia kwamba mwishoni mwa wiki iliyopita walipata taarifa ya mdomo ya kuwepo kwa ongezeko la tozo ya ushuru kutoka dola 152 hadi dola 500 za Kimarekani kwa kila roli.
Sasa alipopelekewa mic ya Clouds FM Dodoma, Dk. TIZEBA kasema wanaendelea na mazungumzo na Serikali ya Rwanda ili kuona viwango bora vitakavyokuwa vikitozwa bila kuwaumiza wasafirishaji lakini pia tofauti ya ushuru wa barabara unaotozwa kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki inatokana na uimara wa barabara husika.
Jana September 2 2013 Serikali ya Rwanda ilitangaza ushuru mpya wa barabara kwa magari yenye usajili wa Tanzania yaliyokuwa yakiingia Rwanda na kuyataka kulipa Dola 500 badala ya Dola 152 zilizokua zinalipwa mwanzoni kitendo ambacho kilisababisha foleni ya magari kwenye eneo la Rusumo mpaka wa nchi hizi mbili.

No comments: