Akerwa uzee kushikiwa bango
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema uzee haupaswi kuwa kigezo cha kumtosa mtu anayetaka kugombea urais 2015, kwa vile fursa hiyo siyo sawa na kutafuta uzuri ‘urembo’ bali kumtafuta kiongozi atakayebadilisha nchi irudi kwenye uadilifu ambao umepotea.
Sitta alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Medani za Siasa na Uchumi kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Star Tv kuhusu siasa za Tanzania.
“Kuna suala la kutafuta vigezo ambavyo havina maana, wengine wanazungumzia juu ya ujana na uzee, haya siyo mashindano ya uzuri tunazungumzia kiongozi wa nchi, katika hali ngumu tuliyokuwa nayo kweli unaweza kujaribu urais,” alisema.
Alisema wapo wanaosema umri wa kugombea urais upunguzwe uwe miaka 30 na kutolea mfano wa nchi kama Marekani bila kufanya utafiti wa kina katika nchi hiyo.
Sitta alisema nchi kama Marekani inaweza ikaendelea kwa sababu ina taasisi za msingi kama sekta binafsi ambazo zinaingizia serikali fedha hivyo katika nchi hiyo huhitaji rais wa ajabu sababu hata suala la chanjo kwa watoto serikali haihusiki bali limebaki kuwa la sekta binafsi tofauti na hapa kwetu.
Aliongeza kuwa vigezo vya ujana na uzee ni vya ajabu, kinachotakiwa ni kumpata mtu mwenye uwezo wa kuiongoza nchi anayejua nyufa zilizopo na mwenye maarifa ya kujua katika jambo fulani tumekosea wapi.
“Mwelekeo wangu mtu wa chini ya miaka 40 itakuwa ngumu kuongoza nchi katika hali tulipofikia na kwamba kazi kubwa ni kubadilisha nchi irudi kwenye uadilifu maana tulishajisahau mno tukawaacha viongozi wakafanya biashara wakiwa ndani ya madaraka na sasa ni mabilionea,” alisema.
Sitta ambaye amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa wanasiasa wanaoutamani urais ifikapo mwaka 2015, alisema wakati ukifika yeye kama mwanasiasa atapima upepo kama awanie au la.
“Mwanasiasa unapima hali halisi ilvyo, wagombea ni nani? Je, nchi inatamka tamka jina langu, huwezi kujitosa tu wakati hueleweki?” alisema.
Akizungumzia vyama vya upinzani, alisema kwa kiasi fulani vinaendelea kupata nguvu ingawa vingeweza kupata umaarufu zaidi kama vingekuwa vichache kuliko hivi sasa vilivyo vingi.
“Upinzani tunapenda uwepo, lakini hali ya kuchochea uongo na kuponda kila kitu siyo sahihi, mfano huwezi kusema hakuna jambo lolote la maendeleo lililofanywa hapa nchini, wakati zipo barabara, viwanja vya ndege na mambo kadhaa yaliyofanywa na serikali,” alisema.
Kuhusu uadilifu wa viongozi, alisema hivi sasa limeanza kufanywa kama jambo la kawaida kununua watu kwa fedha na ndiyo maana kiongozi wa kisiasa anayekuwa na fedha anasifiwa sana tofauti na zamani ukiwa na fedha unatiliwa shaka.
Sitta alisema kutokana hali hiyo kuna hatari ya mwaka 2015 kupata rais aliyebebwa na matajiri na hivyo atakuwa anawatumikia matajiri ambao ndiyo wamemwezesha kupata urais kuliko maskini.
Aliongeza kuwa uwezo wa nchi ni mkubwa sana kuweza kubadilisha hali ya maisha, lakini hilo halifanyiki na ndiyo maana vijana wengi hawana ajira na sasa wamejiingiza katika shughuli ambazo nyingine ni za hatari.
“Hivi sasa tuna vijana takribani 600 katika mabara kadhaa ambao wapo kwenye jela za nchi hizo ambao baadhi yao wamekamatwa kwa kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, vijana wanajiingiza kwenye biashara hiyo sababu hapa nchini ili uonekane wa muhimu kwa jamii lazima uwe na pesa hata kama ni chafu.
Waziri Sitta aliyasema hayo wakati ambao baadhi ya wabunge vijana wanataka umri wa mgombea urais uanzie miaka 35 kutoka miaka 41 na wa mpigakura uwe miaka 16 badala ya 18 ya sasa.
Mbali na Sitta makada wengine wa CCM wanaotajwa kuwa na ndoto za urais ingawa kwa nyakati tofauti wamekataa kuthibitisha au kukanusha, ni Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bernard Membe; Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CCM na Naibu Katibu Mkuu wa UN Mstaafu, Dk. Asha Rose Migiro; Spika wa Bunge, Anne Makinda na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Kazi, Profesa Anna Tibaijuka.
Pia yumo Waziri wa Uchunguzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekonolojia, January Makamba; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdallah Kigoda ambaye mwaka 2005 alijaribu bahati yake lakini hakufanikiwa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment