Mmiliki wa hoteli ya Gold Crest ya jijini Mwanza ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini Bw. Mathias Erasto akizungumza machache wakati wa kuikaribisha Skylight Band jijini Mwanza kwenye Fiesta After Party iliyofanyika kwenye hoteli yake mwishoni mwa Juma ambapo pia ameahidi ushirikiano wa karibu sana na Skylight Band na kuwaahidi zaidi wakazi wa Mwanza burudani zaidi kwa kuwaletea wasanii kutoka ndani na nje ya nchi.Kushoto ni Mmiliki wa Skylight Band Dr. Sebastian Ndege a.k.a Jembe ni Jembe
Aneth Kushaba AK 47 sambamba na Mary Lucos wakitoa burudani kwa wakazi wa Mwanza kwenye After Party ya Fiesta iliyofanyika jijini Mwanza siku ya Jumapili kwenye Hoteli ya Gold Crest.
Binti mwenye kipaji cha aina yake Mary Lucos akiwapa raha wakazi wa Mwanza.
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo akitawala jukwaa huku akipewa sapoti na Mary Lucos pamoja na Digna ndani ya Gold Crest Hotel.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Sehemu ya umati wa wakazi wa Mwanza waliojitokeza kushuhudia burudani ya Skylight Band.
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake ukumbini.
Aneth Kushaba AK 47 akimpagawisha shabiki wake katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza.
Ebwana hii Band ni noma aisee...Wadau wakiwa VIP wakiangalia burudani ya Skylight Band na hawakuamini macho yao.
Hapana Chezea Skylight Band wewe....
Mmiliki wa hoteli ya Gold Crest ya jijini Mwanza ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini Bw. Mathias Erasto akionyesha umahiri wake wa kusakata sebene la Skylight Band ndani ya ukumbi wa Hoteli hiyo.
Shabiki wa kizungu na mdau wa jijini Mwanza wakionekana kuchizika na Skylight Band.
Msanii Diamond Platinumz akiingia ukumbi kupiga show jukwaa moja na Skylight Band kwa mara ya kwanza kuimba na Live Band jijini Mwanza.
Wakazi wa jiji la Mwanza wakimshangilia Diamond alipokuwa akiingia ukumbini huku wengine wakimpiga picha.
Msanii nyota wa Bongo Flava Diamond Platinumz akitoa burudani kwa wakazi wa Mwanza kwenye Fiesta After Party na Live Band ya Skylight. Kulia ni Sam Mapenzi wa Skylight Band wakiimba pamoja na Diamond.
Diamond Platinumz akiwacheza mashabiki wake wa Mwanza Style ya Ngolongolo kwenye wimbo wake mpya unaobamba na kufahamika kwa jina la "My Number One".
Diamond Platinumz akicheza style yake ya Ngololo na mashabiki wake wa Mwanza ndani ya Gold Crest Hotel.
Wengine walipanda jukwaani na kupiga nae picha za ukumbusho.
Ukumbi ulifurika ni balaaa....
Msanii wa muziki nchini Linah Sanga akitoa burudani kwenye Fiesta After Party sambamba na Mary Lucos wa Skylight Band ndani ya Gold Crest Hotel.
Linah akicheza na mashabiki wake wa jijini Mwanza.
Linah ft Sam Mapenzi wa Skylight Band wakitoa burudani kwenye Fiesta After Party iliyofanyika mwishoni mwa Juma ndani ya Gold Crest Hotel.
Msanii Richie Mavoko na Skylight Band wakipagawisha wakazi wa Mwanza.
Wakazi wa jijini Mwanza wakinywa na kufurahi huku burudani ya Skylight Band ikiendelea.
Warembo wa Ukweeee walipamba ukumbi wa hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza wakati wa Fiesta After Party jijini Mwanza.
Wengine wakiwa wamekaa kwenye kushuhudia burudani ya kukata na shoka iliyokuwa ikitolewa na Skylight Band.
Jukwaa la Skylight Band lilipambwa na Richi Mavoko pamoja na Linah kama wanavyoonekana Back Stage na Sam Mapenzi wa Skylight Band.
Palikuwa hapatoshi Gold Crest Hoteli.
Wadau wa Mwanza wakishow love mbele ya camera yetu.
Yachuma mimi nataka mukanda ya chuma chuma....Style mpya ya Skylight Band inayofahamika kama Yachuma chuma.
No comments:
Post a Comment