Isabelle ni mwanawe rais wa Angola Jose Edwardo Dos Santos
Afrika ina mabilionea 55 idadi hii ikiwa kubwa zaidi ya ile iliyosemekana siku za nyuma. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya jarida la Ventures financial nchini Nigeria.
Kati ya hawa mabilionea watatu ni wanawake , mamake Rais wa Kenya , mwanawe rais wa Angola na mfanyabiashara wa mafuta pamoja na mitindo ya mavazi nchini Nigeria.
Mwanamume tajiri zaidi ni Aliko Dangote,wa Nigeria mwenye mali ya thamani ya dola bilioni 20 katika biashara zake.
Hii bila shaka itazua mjadala kuhusu pengo lililopo kati ya matajiri na maskini barani Afrika.
Mnamo mwezi Aprili, benki ya dunia ilisema kuwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini mkubwa barani Afrika imeongezeka katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita kutoka watu milioni 205 hadi watu milioni 414 .
Ripoti iliyotolewa awali, na shirika la utafiti la Afrobarometer ilipendekeza kuwa ukuwaji wa kiuchumi barani Afrika unawanufaisha wachache sana.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Tomi Oladipo, hii ni mara ya kwanza jarida lenye ushawishi la Ventures Nigeria kuchapisha orodha ya waafrika wenye utajiri mkubwa,
Mabilionea hao 55 waliotajwa na jarida hilo ni wengi zaidi kuliko idadi iliyochapishwa na jarida la maswala ya kifedha la Marekani mwaka jana.
Watafiti wa jarida hilo walitumia mbinu tofauti na jarida zengine kufanya utafiti wao na ndio maana wakaja kugundua idadi hiyo kubwa ya matajiri wa kiafrika.
Kwa mujibu wa jarida hilo, utajiri wa mabilionea hawa ukijumlishwa unakuwa wenye thamani ya dola bilioni 143.88 kila mmoja akiwa na utajiri wa dola bilioni 2.6.
Kati ya mabioleana hawa, 20 ni wa Nigeria, 9 kutoka Afrika Kusini, wanane ni raia wa Misri.
Mwanamke tajiri zaidi ni Folorunsho Alakija, wa Nigeria akiwa na mali yenye thamani ya dola bilioni 7.3 kwa sababu ya biashara zake za mafuta. Pia alisomea masomo ya mitindo mjini London na hata kumshonea nguo Maryam Babangida, marehemu mkewe aliyekuwa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria, Ibrahim Babangida..
Isabel Dos Santos, muwekezaji wa Angolan na mwanawe rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos,pamoja na mama Ngina Kenyatta mamake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia wamo kwenye orodha hiyo.
Mfanyabiashara wa Afrika Kusini Allan Gray aliyesomea chuo kikuu cha Havard, ndiye tajiri mkubwa nchini Afrika Kusini akiwa na mali yenye thamani ya dola bilioni 8.5.
Nathan Kirsh, kutoka Swaziland na mwenye mali katika sekta ya ujenzi , pia alikuwa kwenye orodha hiyo. Mali yake ni ya thamani ya dola bilioni 3.6 na ana biashara mjini London na New York.
Kwa mujibu wa jarida hilo, idadi hii ya mabilionea huenda ni ndogo kwa sababu waafrika hawaamini sana jambo ya kujivunia utajiri wakati unaishi miongoni mwa watu maskini
No comments:
Post a Comment