ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 2, 2013

BINTI AMKATAA MWANAE BAADA YA KUMZAA KISA HANA UWEZO WA KUMLEA, AKILELEWA NA KUJA KUWA KAMA SERENA WILLIAM SIJE KWENDA KWAPILATO

Mama wa mtoto ndio huyu pichani anadai hana wazazi walifariki.Akawa analelewa na dada yake huko Sinza na akapata ujauzito.
Baada ya kupata ujauzito dada akamfukuza nyumbani na aliyempa ujauzito akamkataa.
Ni katoto ka kike kenye afya teleee na ana siku tatu tu toka kuzaliwa. Bahati mbaya amezaliwa katika mazingira ambayo mama yake hayupo tayari kumlea na ilikuwa amtupe wasamaria wema wakaokoa jahazi.
Inavyosemekana mama wa mtoto alienda dispensary kuchoma sindano mimba itoke.Bahati nzuri mtoto siku zilikuwa zimetimia akamzaa.Alipozaliwa na kuwa hai mama mtoto akawa hamtaki anataka kumtupa.Mama wa mtoto hamtaki kabisaaaa mwanae.
Kina mama pichani wakimwogesha mtoto baada ya kuzuia zoezi la mama kutupa mtoto
Kina mama baada ya kuzima zoezi la mtoto kutupwa wakakaa na binti kuelewa nini kinamsibu. Wakamuogesha mtoto na mama yake pia akaogeshwa. Akapewa maneno ya kumsaidia kisaikolojia lakini haikusaidia mama msimamo wake ukawa ule ule. Mama aliyekuwa akimuogesha mtoto yupo radhi kumchukua mtoto na kumlea kama wa kwake maana mama yake hamtaki.
Niliwahi kuona movie zamani inafanania na hili binti mdogo alipata ujauzito lakini hakuwa tayari kuwa mama na akamtoa mwanae kwa mtu na mkewe waliokuwa wanamatatizo ya kupata mtoto. Alimtoa kwasababu yeye asingeweza kulea na kumpa mahitaji yote. Yule baba na mkewe ndio walikuwa wakihitaji mtoto zaidi yake.

2 comments:

Anonymous said...

Binti unamatatizo unatakiwa usaidiwe, Mbona hukwenda ITV au DTV walau hata kwa wadau ili ukachangiwa!! Umebeba miezi tisa leo unagoma nani alikuwa anakusaidia na kwenda clinic? Je unaacha ili ukarudie tena sio. Acha ulimbukieni.

Anonymous said...

mimi jamani namuomba awe mwanangu maana nahitaji mtoto sana.Nipo dodoma please