Mhe. Balozi Liberata Mulaula katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei wakati wageni wakiingia kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya kutangaza huduma mpya za kibenki kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite.
Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiingia kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kulikofanyika hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB Bank Jumatano Oct 9, 2013 kwa ajili ya kutambulisha huduma mpya za Benki hiyo kwa ajili ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwatamburisha waheshimiwa wageni kwa baadhi ya Watanzania walofika kusikiliza huduma mpya za Benki ya CRDB kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite na baadae kumkaribisha mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei kuongea na WanDMV kwa niaba ya WanaDiaspora.
Mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank, Dkt Charles Kimei akielezea huduma hizo mpya ambazo ni JIJENGE (Mortgage Finance) na FAHARI HUDUMA (Argent Banking) na pia alielezea maboresho ya hudma ya Tanzanite ikiwemo mteja anapofkisha kiasi fulani cha pesa kwenye akaunti yake hakutakuwa na makato ya aina yeyote yatakayokatwa kila mwezi.
Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiongea machache na kuwaambia wanaDMV wajisikie wapo Tanzania na salama kwani amekuja na ujumbe mzito unaowakilisha Bara na visiwani na baadae kumshukuru Mhe. Balozi Mulamula kwa makaribisho mazuri na CRDB Bank kwa kuandaa hafla hiyo fupi iliyofanyikia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Jumatano Oct 9, 2013 jioni.
Waziri wa Fedha na Uchumi akiongoza ujumbe wake kwenye chakula cha jioni.
Duputy Governor Economic & Financial Policies Dkt. Natu El- maamry Mwamba akijiatia chakula cha jioni.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula nae akijipatia chakula cha jioni.
Kulia ni Waziri wa Fedha na Uchumi Zanzaibar Mhe. Yussuf Mzee akibadilishana mawili matatu toka kushoto ni Mariam Mkama, Love Maganga na Tully Esther Mwambapa ambaye nia Director of Marketing, Reserch and Customer Service wa CRDB Bank.
Mkurugenzi mkuu wa TRA Harry Kitilya (kati) akibadilishana mawili matatu na Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Colonel Adolph Mutta (kushoto) na Afisa Ubalozi Dkt. Switebert Mkama.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Mshereheshaji Afisa Ubalozi Suleiman Saleh
Juu na chini wadau wakifuatilia mawili matatu kutoka kwa watoa hutuba.
Wageni waheshimiwa wakipata chakula cha jioni.
Juu na chini ni Warizi wa Fedha na Uchumi na ujumbe wake wakibadilishana mawili matatu na Balozi Liberata Mulamula baada ya kumaliza kupata chakula cha jioni kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB Bank kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwaaga wageni wake mara lipomalizika hafla hiyo picha Mhe. Liberata Mulamula akiagana na Gavana wa Bank Of Tanzania Prof. Beno. Ndulu kushoto ni Baraka Munisi ambaye ni Mortgage Finance Specialist.
Baraka Munisi (kushoto akiongea jambo na Prof Benno Ndulu huku Baraka Daudi(kati) ski sikiliza.
3 comments:
sawa crdb lakini kabla ya kuendelea kujinadi huku nje jaribuni kubadilika hasa kwenye customer care. Ni ukweli usiopingika customer care yenu ni zero hasa kwa watu walioko nje!..niliwahi kusikia stories sikuamini hadi mimi mwenyewe nilipopata experience mbaya sana ya customer care yenu. Japo nilijatahidi kuandika email ya malalamiko kwenu binafsi Mr. Kimei & Ms Tully kupitia address zenu mlizoweka kwenye website ya crdb but hakuna hata aliye-acknowledge na kunijibu..nilichukizwa sana!
Vitu kama hivi labda ninyi huko nyumbani mnaona ni sawa na sahihi lakini kwetu sisi huku ni one of the worst customer service..hata kama huna solution kwa customer ni muhimu ku-acknowledge kupata malalamiko yake!..Mnaweza hata kuchek email zenu kuhakiki haya ninayoyasema hapa maana ziliwafikia!
amos
Mdau Customer Care Ni Janga la Taifa kwa ujumla hususani sector za Banks, na Hospitals!!! Inatia Kinyaa kwamba muhudumu wa bank anaongea na mteja Kama mtoto wake nyumbani au Kama vile anasumbua!!!!! Yaani hapa nyumbani wanaitaji customer service lessons kwa hali na mali! Wmesahau kuwa " mteja Ni mfalme" na bila wateja wasingekuwa na mishahara maana kungekuwa hakuna kazi za wao kufanya this includes all the top executives also not only the low income positions! Inasikitisha sana sana sana! Kwenye sector za serikali Kama Tanesco ndo hawafaiiii kabisa ikija customer Care!!! MAJANgA!
wanafurahia vinywaji,picha na chakula but hawafanyi kazi yoyote ile yaani hizi picha wala mkutano wao hausaidii chochote ni wabovu kabisa wa kazi,hebu tuondoleeni upuuzi huu.
Post a Comment