ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 11, 2013

Dr. Wilibrod Slaa akiendelea na ziara yake iliyopewa jina la “Vision Tanzania” leo ametembelea chuo kikuu cha Indiana

Mwanafunzi wa Kitanzania katika chuo cha Indiana akimpokea Dr. Slaa
Kutoka Kushoto, Mwanafunzi wa Kitanzania, Dr. Slaa, mwanajeshi mtafiti pamoja na Mwenzie ambaye ndiye kiongozi wa utafiti
Dr. Slaa akikagua mtambo wa utafiti uliogunduliwa na Wanafunzi na walimu katika chuo cha Utafiti wa Indiana. Mtambo ni wa kutengenezea gesi ya hydrogen pamoja na umeme mbadala (renewable energy) unaopatikana kutokana na takataka
Meya pamoja na mkuu wa polisi nao walikuja kumuona Dr. Slaa na kumkaribisha kwenye jiji lao
Dr. Slaa baadae jioni alikutana na wakurugenzi wa mashirika makubwa ya nishati (renewable energy) nchini marekani ambao wako tayari kufanya kazi na CHADEMA kuiletea Tanzania umeme wa bei nafuu. Baadhi ya hawa wawekezaji wamewahi kuja Tanzania lakini Tanesco kama kawaida yao wakawakwamisha. Chadema inajipanga kuwaletea watanzania unafuu wanaoulilia
Viongozi wa chuo kwenye picha ya pamoja na Dr. Slaa

No comments: