Mfuko wa Pensheni wa PSPF umeandaa semina maalum kwa wadau wa tasnia ya sanaa na michezo katika mgahawa wa Akemi katika jengo la Golden Jubilee Tower yalipo makao makuu yao ili kuwajulisha wadau hawa kuwa mfuko huu ni wa kila mtu si kwa waajiriwa pekee au wafanyakazi. Mtu yeyote anaweza jiunga na mfuko huu, kuanzia mjasiliamali, mchezaji, mwanamitindo, mbunifu,muigizaji nk.
Meneja wa mawasiliano na masoko Bi Constantina Martin akiwaelezea wadau wa sanaa kuhusu mfuko wa pension wadau tuliohudhuria wakiwemo wasanii,wanamichezo,mamc,wanamitindo nk juu ya mfuko huu ambao hata waliojiajiri wanaweza kujiunga nao na zaidi ya mafao ua uzeeni pia kuna nyumba humo na inaweza kuwa dhamana ya mkopo wa nyumba kutoka bank.
Mkurugenzi wa PSPF Mr Adam Mayingu nae alikaribisha wadau waufahamu mfuko huu kwa kuwa una manufaa si kwa wakazi wa tanzania tu hata mlioko nje ya nchi mfuko huu unawahusu tena saana mambo ya kutumia nyumba ujengewe mwisho wa siku wakuta nyumba hewa hakuna PSPF wananyumba na ukijiunga watakuwezesha upate mortgage.
1 comment:
Weka anuani na simu zenu kwa mawasiliano zaidi. Kuna watu tuna interest kujua zaidi mwafanyaje hapo lwrnye swala la nyumba. Mdau.
Post a Comment