ANGALIA LIVE NEWS

Friday, October 4, 2013

Ghasia baada ya mauaji Mombasa

Salim Adbi pekee ndiye aliyenusurika kifo
Taarifa kutoka mjini Mombasa pwani ya Kenya zinasema kuwa vijana wameteketeza kanisa katikaghasia ambzo zimezuka kufutioa kuuwa kwa muhuburi wa kiisilamu. Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa keenye ghasia hizo.
Sheikh Ibrahim Omar aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa na washirika wake watatu.
Polisi wamesema kuwa muhubiri huyo alikuwa amehubiri katika msikiti uliohusishwa na wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab.
Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku wa kuamkia leo huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo.
Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi. Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa wanarejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.
Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama Al Shabaab.
Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab

Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo.

Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa

Kundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ya kigaidi.

Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Shabab na baadhi ya waisilamu walioshutumu polisi waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu wala.

Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.

9 comments:

Anonymous said...

Wakenya wanataka kupoteza umma wa waislam katik Nchi ya Kenya lakin kwa uwezo wake aliye waletea dini ya Haki Allah(sw)hawatofanikiwa na katika Pwani nzima ya kenya kila siku wanazaliwa masheikh wapyaa...ukiuwa huyu anakuja huyu watachokaaa wenyewe ni kama kipindi cha Manabii akifa huyu anakuja huyu.

uislamu ni dini ya haki na ya kweli ndo maana ulimwengu mzima unapiga vita uislamu na kuwababikizia uongo wa kuwaita magaidi na ndo maana utaona popote pale panapotoka mafuta na rasilimali wanazo zitaka mabeberu basi kuna waislamu.

inshallah Allah atawaokoa waislamu wote ulimwenguni na njama za maadui zao amin amin amin

Anonymous said...

Inalilahi wa Inailaihi Rajiun.
Kenya wanajipalilia mkaa,
wanayoyafanya yatawarudia.
Kwa damu ya waislam kwao haina thamani.
Malipo yanaanzia hapahapa duniani.

Anonymous said...

serikali ya kenya inawatesa sana waislam masheikh wa mombasa ndo maanake wanataka kujitenga.baada ya tukio la westgate wameanza kuwashtumu masheikh wa mombasa kitu ambacho kinazidisha chuki kwa waislam kuishtumu serikali yao.kuna kundi la mungiki linaua wakenya wengi lakini hawaitwi magaid,marekan anaua watu kili leo iraq,afghanistan,syria lakini eti wanapambana na magaid.naunga mkono alshabab kupambana na serikal dhalim ya marekan na vibaraka wake wa kenya

Anonymous said...

Bila shaka mitihani, maumivu na dhulma dhidi ya waislamu ni jambo la kihistoria. Tunasema mitihani ni sunna ya wachamungu. Uzuri ni kwamba historia inaonyesha muda wote wa mateso waliopitia waislamu mwisho wake wamekuwa washindi. Silaha kubwa sana katika vita hii ni kuwa na subra na sio kupetuka mipaka kwani ni wazi tukivuka mipaka aliyotuwekea Mungu kama waislamu adhabu yetu itakuwa kubwa hapahapa duniani na kesho akhera. Wenzetu wameshakata tamaa na maisha ya akhera na wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha nasi tunakuwa kama wao. Dunia sasa imepanga ajenda kali dhidi ya uislamu kwa mgongo wa ugaidi. Ni vita nzito sana kwetu waislamu bila uvumilivu tutajikuta tunaingia katika mtego wao. Matukio ya kuudhi na kutia hasira kama haya yalishatokea tena kwa kiwango kisicho na mfano zama za mtume s.a.w ila wao walifanya subra na mwisho ushindi ukawa upande wao. Tuendelee na subra nusra ya Allah haipo mbali kwa waumini. Inshallah.

Anonymous said...

wanadamu tunapaswa kuwa makini sana na hii kitu inaitwa ugaidi.somebody is playing double agent akichochea waislam na wakristo kwa hate doctrines na matukio.huyu evil agent yupo ndani ya dini zetu akijjita mkristo kwa wakristo na muislam kwa waislam.Kenya inaelekea kuuvaa huu mtego na machafuko makubwa sana yanawasubiri wasipostukia mchezo huu mchafu wa neo-colonialism.Tanzania wananchi wamekuwa wazito kupokea hii kitu all of christians na majority of muslims hawataki umwagaji damu Tz.Mungu awasaidie mbaki hivyo hivyo,mnaonekana wajinga lakini hapo ndipo hekima ya watz ilipo.hii vita sio yenu wakristo na waislam,yuko mtu analazimisha iwe yenu mmwage damu zenu.msiuvae mtego huu,waacheni wamwagane damu wenyewe ili muwajue hao kizazi cha nyoka,wana wa laana wasiopenda amani.

Anonymous said...

It must be the fury of the Kenyan Intelligence Services, for those people fanning the fires of Al Shabab.

Anonymous said...

Chuki zisizo na msingi zipo kwa mtu aliye kizani, akipata mwanga anapona ugonjwa huo.

Anonymous said...

Bila shaka mitihani, maumivu na dhulma dhidi ya waislamu ni jambo la kihistoria. Tunasema mitihani ni sunna ya wachamungu. Uzuri ni kwamba historia inaonyesha muda wote wa mateso waliopitia waislamu mwisho wake wamekuwa washindi. Silaha kubwa sana katika vita hii ni kuwa na subra na sio kupetuka mipaka kwani ni wazi tukivuka mipaka aliyotuwekea Mungu kama waislamu adhabu yetu itakuwa kubwa hapahapa duniani na kesho akhera. Wenzetu wameshakata tamaa na maisha ya akhera na wanafanya kila liwezekanalo kuhakikisha nasi tunakuwa kama wao. Dunia sasa imepanga ajenda kali dhidi ya uislamu kwa mgongo wa ugaidi. Ni vita nzito sana kwetu waislamu bila uvumilivu tutajikuta tunaingia katika mtego wao. Matukio ya kuudhi na kutia hasira kama haya yalishatokea tena kwa kiwango kisicho na mfano zama za mtume s.a.w ila wao walifanya subra na mwisho ushindi ukawa upande wao. Tusiunge mkono matendo ya kidhalimu kama ya alshabaab mfano wa pale wastagate(iff wanahusika). Tuendelee na subra nusra ya Allah haipo mbali kwa waumini. Inshallah.

Anonymous said...

Kanisa na Serkali ni kitu kimoja.