ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 12, 2013

HABARI YA KUSIKITISHA: HAWAKUOMBA KUJA DUNIANI KUTESAKA?

Agustino Steven (8) akiandaa ugali ale na dada yake
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakichambua mboga aina ya mchicha 
Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Agustino Steven (8) akipika mchicha
Hii ndiyo sahani yao wanayotumia kwa ajili ya chakula 
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) hapa wakila chakula walichopika wenyewe
Unga pamoja na maharaja
Hili ndilo sanduku lao
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakiwa nje ya nyumba wanayoishi

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi matano bila huduma za msingi.

Watoto hao wamefahamika kwa majina ya Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema Wazazi wao waliwaacha kwenye nyumba ya kupanga tangu mwezi wa Mei mwaka huu ambapo Baba inasadikika alielekea Umalila Mbeya Vijijini ambako inasemekana ameoa mke mwingine.

Wamesema Mama yao alielekea Mbozi ambako pia naye inasadikika ameolewa na mwanaume mwingine hivyo kuwaacha watoto bila kuwa na huduma za msingi kama Chakula na mavazi huku wakiwa wameachiwa Nyumba mtaa wa Jakaranda Airport.

Aidha watoto hao waligundulika baada ya kukutwa mitaani wakitafuta riziki kwa kuzoa taka kwenye majumba ya watu kisha kupeleka majalalani kwa ujira wa kati ya shilingi 200 na 500 ambazo huzitumia kununua mahitaji ya nyumbani pamoja na kujipikia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Amesema majirani pia waendelee kuwa karibu na watoto hao hadi pale wazazi wao watakapopatikana kwa kuwahudumia na kuhakikisha wanaendelea na masomo kama kawaida.

Amesema kitendo kilichofanywa na wazazi hao ni cha kinyama hivyo wakipatikana hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ambapo pia alitoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kikatili.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa mbeyayetu.blogspot.com umebaini kuwa Wazazi hao wanatabia kama hiyo kutokana na kuwahi kumtelekeza binti yao mwenye umri wa miaka 17 aliyefahamika kwa jina la Salome Steven ambaye hakuwahi kupelekwa shule hivyo kuachiwa jukumu la kuwalea wadogo zake.

Kutokana na ugumu wa maisha binti huyo katika harakati za kutafuta chochote kwa ajili ya wadogo zake ameishia kuzalishwa mtoto wa kiume ambaye ana mwezi mmoja sasa na kuwakimbia wadogo zake nay eye kukimbilia kwa rafiki yake.

Pia Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia limeamua kulifuatilia suala hilo kwa kumtafuta kijana aliyemzalisha binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Hezron ambaye imedaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwenye nyumba ya kulala wageni(Gesti ).

Na mbeya yetu

7 comments:

Anonymous said...

Mmmmmmmh binadamu kweli tuna roho ngumu! Sishangai sana kwa desturi yetu watanzania wengi ndo tabia zetu. Hoja yangu kwako wewe muhusika ulie tembelea hao watoto na kuona hali halisi waliyonayo. Umeondoka na kuwaomba majirani wawa angalie na hali halisi inajulikana kuwa kuna wizara husika za jamiibna maendeleo ya watoto kwa nini wasihusishwe kuwasaidia wakati mkiendelea na utaratibu wa kuwasaka wazazi wahusika kuliko kuwaomba majirani wawa angalie.? Hebu tuwe na roho za kibinadamu jamani. Ni malaika hao hawana kosa duniani humu. Wengi tumeyaoitia mateso lakini wazazi hawakututupa kama hivyo. Naomba njia ya mawasiliano namba ya kuwasaidia na uhakiki wa kuwa msaada wangu umewafikia. Mdau. Email yangu nyali16@yahoo.co.uk

Anonymous said...

Sawa wazazi watatafuta mwisho wake watafungwa.Je idara ya watoto iko wapi kusaidia hawa watoto?Habari inavyoonyesha kuwa wameomba jirani ieendelee kuwaangalia.Jamani kwa nini kusiwe na nyumba maalum kwa ajili ya maswala kama haya?Jamani inasikitisha.

Anonymous said...

Kuna wazazi wengine utadhani walilazimushwa kuzaa...kama wanapenda mchezo basi watumie kinga sio kuleta viumbe humu duniani halafu kiwatesa nyoko zao

Anonymous said...

why this official let the burden to the neighbors? The leaders should step up and rescuing this precious kids.I 'm sure neighbors will take advantage to use them as their laborer.

Anonymous said...

mimi naitwa Irene rouse. hii habari imenisikitisha sana. ningependa kujua, ni njia gani naweza kutumia kuwasaidia hawa watoto. naomba mnijulishe jamani. mimi nina watoto umri huu. inaniuma sana kuona watoto wanateseka . my email ni ireneakinyirobert@yahoo.com.

Anonymous said...

uliyeuliza wizara ya jamii na maendeleo na watoto iko wapi??..JIBU ni kuwa wapo busy na vikao na safari zenye perdiem na maposho..!..

unashangaa hili la wizara ya watoto kuwa mbali??mbona hushangai wale watoto wadogo ombaomba wanaogonga madirisha ya magari kwenye traffic jams pale darisalama ambapo ndipo wizara husika ipo??au maybe waziri&wakurugenzi husika wakiwa kwenye mashangingi yao ni vigumu kuwaona wale watoto maana vioo vyao ni tinted!

serikali ya tz inasikitisha sana linapokuja suala la kuwa responsible na watoto wake..wangejua kuwa watoto duniani kote ni mali ya serikali..!..poleni sana watoto na Mungu atawasaidia

mdau
Ujeruman

Anonymous said...

watoto si mali ya serikali watoto ni mali ya mungu, mungu tu peke ndo atakaye weza kuwatunza hawa watoto hakuna zaidi yake.