Wednesday, October 23, 2013

HASHEEM THABIT ASIMAMISHWA KUCHEZA MECHI MOJA BILA KULIPA FINE KWA KOSA LA KUMPIGA KICHWA MCHEZAJI WA TEAM PINZANI

Mcheza kikapu ‘Hasheem Thabit’ raia wa Tanzania ambaye anachezea timu ya Oklahoma City Thunder inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani maarufu kama NBA amejikuta akitumikia adhabu aliyopewa na timu yake hiyo ya kutocheza mechi moja na kukatwa mshahara wake baada ya kumpiga kichwa mchezaji mwenzake wa timu ya New Orleans ‘Greg Stiemsma’ katika mchezo uliozikutanisha timu hizo mbili mwishoni mwa wiki ambapo New Orleans iliibuka na ushindi wa jumla ya vikapu 105 kwa 102 dhidi ya Thunder.

Kwa mujibu wa taarifa zinasema kwamba ikiwa zimebakia dakika takribani 26 kuweza kumalizika kwa kipindi cha kwanza, Timu anayochezea Thabit ya Thunder ilikuwa inaongoza kwa vikapu 54 kwa 51 dhid ya Orleans, Thabit alijaribu kumkaba ‘Stiemsma’ hali iliyozua ugomvi baina ya wachezaji hao wawili na kuanza kupigana vikumbo hali iliyopelekea Hasheem Thabit kumpiga kichwa mlinzi wa kati wa New Orleans ‘Greg Stiemsma’ na muamuzi wa mchezo huo kupuliza kipenga kuashiria kusimamisha mchezo na kutoa foul kwa timu hizo huku akiwaamuru wachezaji hao kuendelea na mchezo.

Katika mchezo huo Hasheem Thabit aliweza kushinda Point 2 na rebounds 3 ndani ya dakika 14 alizocheza, hii sio mara ya kwanza kwa Hasheem Thabit kugombana na wachezaji wenzake kwani kipindi cha nyuma aliwahi kurushiana maneno na kutaka kupigana na mchezaji wa timu ya Houston Rockets ‘James Harden’.

Kwa wasiomfahamu Hasheem Thabit ndiye mchezaji anayeongoza kwa urefu katika ligi kuu ya mpira wa kikapu Marekani ya NBA, anakadiriwa kuwa na urefu wa Futi 7.3 ambazo ni sawa na mita 2.21 na pia ni raia kutoka Tanzania.

1 comment:

Anonymous said...

There we go!!!! Hasheem???? Ndo matatizoo ya Watanzania hayo, tunajisahau sana!sasa jamaa kasahau kuwa hii Ni chance inayotokea Mara moja sana katika maisha na Ni bahati isiyojirudia matokeo yake anaenda kupigana uwanjani!!!! Duu! Haya bwana yetu macho tu! Kila la kheri Hasheem Mungu akutangulie.