ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 1, 2013

HILI NDIO TAMKO LA GAZETI LA MWANANCHI BAADA YA KUFUNGIWA KUCHAPISHA HABARI KWA NJIA YA TOVUTI.

Tunasikitika kuwaarifu kuwa kutokana na sababu zisizozuilika, tutashindwa kuendelea kuwaletea habari mpya kupitia tovuti yetu (www.mwananchi.co.tz) na mitandao ya kijamii ya Mwananchi kwa wakati wote ambapo uzalishaji wa gazeti la Mwananchi utakuwa umesitishwa.

Tunasikitika kwa usumbufu wowote utakaosababishwa na hali hii na tunatumaini mtaendelea kuwa nasi wakati wa kipindi 
hiki kigumu cha mpito. Tunatarajia kurejea rasmi hewani na habari moto moto wiki ijayo, Ijumaa, tarehe 11 October.

Tunawakaribisha muendelee kusoma habari zetu za zamani (archives) kwenye tovuti ya Mwananchi na kurasa zetu za Facebook na Twitter ili mzidi kuhabarika.

Pia tunawakaribisha mtembelee tovuti zetu za www.thecitizen.co.tz na www.mwanaspoti.co.tz ambazo zitaendelea kufanya kazi kwa ufanisi, zikiwaletea habari za uhakika na kuaminika kipindi hiki ambapo Mwananchi imefungiwa.

Ahsanteni,

No comments: