ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 23, 2013

Kauli nyingine ya umoja wa vyama vya siasa kuhusu hati ya dharura katiba mpya


Umoja wa vyama vya siasa vyenye wawakilishi bungeni umesema umeridhishwa na maafikiano yaliyofikiwa katika kikao cha pamoja na Rais Jakaya Kikwete na kwamba hatua iliyofikiwa ina mlengo mzuri wa kufanikisha upatikanaji wa katiba bora.

James Mbatia ambae ni mwenyekiti wa huu umoja anasema wameridhishwa na namna Rais JK alivyopokea mapendekezo ya wakuu wa vyama vinavyounda umoja huu na kutoa mustakabali wa kuandaliwa kwa mapendekezo maalum ya dharura ambayo umoja huu utaona yanafaa kuwepo kwenye katiba mpya ijayo kabla ya kuanza kwa bunge maalum la katiba.

Katika kikao kilichofanyika Ikulu Dar es salaam October 15 2013, zaidi ya mapendekezo 10 yaliafikiwa kati ya Rais Kikwete na umoja huu ambapo namkariri Mbatia akisema ‘serikali itaandaa hati ya dharura ili sheria husika irejeshwe bungeni haraka katika mkutano wa bunge unaoanza October 29 2013 ili bunge lifanye marekebisho yanayolalamikiwa na wadau mbalimbali’

Historia inaonyesha kuwa endapo katiba hiyo itapatikana, itakua ni mara ya 15 kufanyika kwa mabadiliko ya katiba Tanzania toka mwaka 1977.

No comments: