ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 23, 2013

Majibu ya Naibu waziri wa Kenya William Ruto kwenye interview CNN


Makamu wa rais wa Kenya amekanusha tuhuma zinazomkabili kwenye Mahakama ya makosa ya kivita ambako amekaririwa akisema “ushahidi unaonyesha kuwa sina hatia yoyote na siku si nyingi ulimwengu utafahamu ukweli uko wapi na tuhuma hizi zitathibitishwa kuwa ni za kutengenezwa tu’

‘Nisingependa kuzungumzia ukweli wa ushahidi huo lakini naamini mashahidi hawa wametengenezwa na wametishiwa ndio wakatoa ushahidi huu, timu yangu ya mawakili itathibitisha kuwa kila kitu sio kweli lakini pia kinachoendelea ICC kwenye Mahakama sio rahisi kudhani kuwa Mahakama hii ina ubaguzi wa rangi’ – Ruto

Kuhusu taarifa za kuendelea kuwepo kwa miili ya watu kwenye jumba la Westgate lililoshambuliwa na magaidi September 2013, Ruto amesema ‘si rahisi kufahamu kuwa kuna watu hawajapatikana hadi sasa, vilevile ishu ya wanajeshi kudaiwa na kuonekana kwenye camera za CCTV wakiiba vitu kwenye maduka ya Westgate wakati wa uokoaji ni bahati mbaya ambapo Rais Uhuru ameunda tume itakayofanya kazi ya kuchunguza kilichotokea na kila mmoja ambaye alifanya kosa hili atapelekwa mbele ya sheria’

Kuhusu Kenya kubadili sera yake juu ya Somalia, Naibu huyu wa Rais akiwa The Hague ameiambia CNN kwamba ‘tulikwenda Somalia kutokana na tishio la ugaidi na tutaendelea kuwepo huko mpaka ugaidi utakapomalizika‘

No comments: