Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza wakati akifungua mjadala wa vijana kuhusu dawa za kulevya, uliofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Mratibu wa mradi wa JEE NIFANYEJE, kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Washington, Bi. Khadija Riyami, akizungumza kabla ya kumkaribisha Maalim Seif, kufungua mjadala wa vijana kuhusu dawa za kulevya, uliofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar. Mradi huo unajihusisha na maamuzi ya kiafya na kijamii kwa vijana.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na vijana wa “Sober houses’ baada ya kufungua mjadala wa vijana kuhusu dawa za kulevya, uliofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar.
1 comment:
riyami jifunike basi japo kidogo vizuri huu ushungi wako jamani ukiwa huko kwenu washington ndo ujifunike hivyo mtoto wa kiislamu
Post a Comment