Martha Shani enzi ya uhai wake
Ndugu zangu Watanzania, DMV imepatwa na msiba wa mwenzetu, mzazi wa watoto watatu wa ndugu yetu, Mtanzania mwenzetu Alex Kassuwi kama mlivyosikia na kusoma kwenye mitandao, Alex Kassuwi amefiwa na kipenzi mke wake na mzazi mwenzake siku ya Jumamosi Oct 19, 2013 kwenye hospitali ya FrederIck marehemu alikokua amekimbizwa kujaribu kuokoa maisha yake baada ya kuanza kujisikia vibaya aliporudi asubuhi ya siku hiyo akitokea kazini.
Kutokana na maelezo ya ndugu wa karibu wa familia, alisema kwamba mara baada ya marehemu kurudi nyumbani alianza matarisho ya kupika vyakula vya Besidei ya mtoto wa dada mmoja anaeitwa Quizela mkazi wa maeneo hayo ya Frederick, Maryland. Kabla hata ya kumaliza matayarisho hayo, ghafla marehemu alianza kujisikia vibaya na kuamua kujilaza kwenye kochi.Muda ule marehemu alipokuwa amejilaza kwenye kochi, mume alielekea madukani kupata mahitaji mengine ya nyumbani huku akiwa amemuacha marehemu na watoto.
Wakati akiwa dukani aliona missed call kutoka nyumbani kabla hajafikiria kuirudisha, simu ilipigwa tena ndipo alipoipokea na kukutana na sauti ya mwanae wa kwanza ikimuambia"baba mama ameanguka chini anatokwa na mapovu mdomoni" habari hii ilimstua sana Alex Kassuwi na kukimbia nyumbani mara moja kujaribu kuokoa maisha ya mzazi mwenzake. Wakati huo yule mtoto wao wa kwanza mwenye umri wa miaka 13 alikua pia amekwisha piga simu 911 kuwataarifu yaliyomkuta mama yake na kuomba msaada wa kujaribu kuokoa maisha ya marehemu kipenzi mama yake na baba alipofika nyumbani alikuwa anawasiliana na wahudumu wa 911 wakijaribu mumuelekeza jinsi ya kumpa marehemu huduma ya kwanza wakati wao wakiwa njiani kuja nyumbani kumchukua marehemu kumuwahisha Hospitali.
Mara baada ya wahudumu wa 911 kufika nyumbani, warijaribu nao kumpatia huduma ya kwanza marehemu na baadae kumkimbiza hospitali ya Frederick kwa matibabu zaidi.
Wakati wahudumu wanaelekea hospitali na Marehemu, Alex Kassuwi aliwapeleka watoto kwa Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Neto na kumuomba awangalie wanae huku yeye akielekea hospitali kwa kulifuata gari la wagonjwa kwa nyuma.
Marehemu alipofikishwa hospitali madaktari walihangaika kujaribu kuokoa maisha yake kwa takribani saa zisizopungua sita na baadae ilipofika saa 11 jioni Martha Shani alitangazwa amefariki Dunia na sababu ya kifo chake madaktari walisema marehemu alikuwa na upungufu wa Patassium iliyofanya mishika inayoyosaidia kusukuma mapigo ya moyo kuwa dhaifu.
Kwa hiyo tunaomba ndugu zetu Watanzania msiba huu ni wetu sote na gharama za kumsafirisha marehemu akiwemo mume wake na watoto zinafikia $19,500 na mpaka jana fedha zilizokusanywa zikiwemo ahadi ni $,4,000, tunatoafauti ya $15,500 ambazo kwa mshikamano tulikuwa nao na sifa yetu kubwa kama Watanzania tunapoamua hatushindwi na jambo. Msiba huu umewagusa wengi wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki hapa Marekani na Tanzania.
Baadae tutaweka account ya marehemu kwa Watanzania waliombali na DMV waweze kutoa rambi rambi zao ilikuwezesha kumsafirisha marehemu na hatimae kufanikisha mzishi yake.
Kwa sasa unaweza kuwasiliana na:
Mariam Mtunguja - 240-422-1852
MV Mtunguja- 240-593-0575
Victor Marwa - 240-515-6436
Dickson Mkama - 301-661-6207
Tino Malinda -240-565-7133
Julis Manase-240-393-8445
Quizella Ntagazwa - 240-602-5011
Faith Isingo - 240-705-1055
Msiba upo:
482 ARWELL CT
FREDERICK, MD,21703
BWANA AMETOA, BWANA AMETWA NA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
5 comments:
What a sad story! Rest in peace Martha.
RIP Martha. Hii iwe changamoto ya kutumia supplemental multi-vitamins. zinasaidia sana
Hebu tufafanulie mdau hapo juu multi vitamin na kifo cha Huyu dada vimeingilianaje? Au comment hii si ya hapa? Au una maanisha nini?.tupe somo la hiyo supplement na sisi tujue ni nini .
Mdau wa mwisho ni kuwa kifo cha dada yetu kilisababishwa na low potassium ambayo ni muhimu sana for heart function and many cellular activities in your body ndo maana mdau kasema tukumbuke kula multivitamins kwani mavyakula tunayokula mengi hayana rutba yamekuwa frozen muda mrefu so ukila vizuri na kula Multivitamins una uhakika kuwa viturubisho vya mwili katika kiwango kinachotakiwa. Nadhani umemwelewa
Jamani ...inauma,na zaidi ya maumivu,hasa kwa mume wa marehemu mungu akupe faraja ya pekee .pole sana .
Post a Comment