Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wazee waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, baada ya kuhutubia katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi uliopo Kata ya Manundu, Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Mstaafu, Mussa Shekimweli na Mwenyekiti wa sasa CCM mkoa wa Tanga, Henry Dafa Shekifu, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi Kata cha Manundu, baada ya kuhutubia katika sherehe hizo zilizofanyika Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, leo.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akivishwa vazi la asili la kabila la Wadigo, na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa Wilaya ya Korogwe, Abdallah Semkiwa, wakati wa sherehe za kilele cha Siku ya Wazee Duniani, zilizofanyika mkoani Tanga.
Sehemu ya wazee waliojitokeza kuhudhuria sherehe hizo.
Sehemu ya wazee waliojitokeza kuhudhuria sherehe hizo.
Wasanii wakitoa burudani ya ngoma ya Mdumange, wakati wa sherehe hizo.
Picha ya pamoja na baadhi ya wazee.
No comments:
Post a Comment