Ndugu wanajumuiya,
Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania DMV, kutoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa kazi kubwa mliyoifanya siku ya tarehe 28 September 2013, kwenye siku G-Festival. Banda la Tanzania liling'ara sana na kuvutia wageni wengi waliokuja na kujionea vitabu vya lugha ya Kiswahili, mavazi yetu na hata vyakula vyetu ambavyo kwa pamoja vilisababisha mistari mirefu. Kwa kifupi, banda la Tanzania lilivutia sana ukilinganisha na mabanda ya nchi nyingine.
Shukrani za pekee ziwaendee walimu wa darasa la Kiswahili ambao walishiriki kikamilifu katika shughuli nzima kuanzia kupanga, kutekeleza na kisha kufanikisha tamasha hili, wanajumuiya walioleta vitu vyao kwa ajili ya kuuza na kuvionyesha, mwandishi pekee wa habari toka Vijimambo, Mheshimiwa Luke, na wale wote kwa namna moja au nyingine walitupa ushirikiano kufanikisha tamasha hilo.
Kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya, naomba kuhitimisha kwa kuwashukuru kila mmoja na kuwatakieni kuendelea na moyo ule ule hata katika matamasha mengine yanayokuja.
Asanteni sana.
Amos Cherehani
KATIBU WA JUMUIYA
No comments:
Post a Comment