Usione anakukatalia ukadhani kweli hata, ndiyo zao kuleta sitaki nataka. Anapokwambia hataki, wakati mwingine siyo kweli kwamba hataki. Inawezekana ni kwa sababu hujamwandaa vizuri kihisia, kwa hiyo hayupo tayari. Anapokugomea, anakuwa anakupa taarifa kwamba unatakiwa umuweke akae chonjo. Ni jukumu lako.
Pengine anakwambia hataki ili tu ujiongeze na kumbembeleza ndipo akubali. Asili ya mwanamke ndani yake kuna asilimia kubwa ya aibu kuliko mwanaume. Anapobe-mbelezwa hujisikia raha, hivyo kumuongezea mshawasha. Usiniambie na hili hulijui!
Kwa bahati nzuri zaidi ni kwamba mwanamke anaposema hataki na kama una uhakika kwamba kichwa chake kipo sawa, jukumu lako ni moja tu, kumchangamsha na kuzipasha moto hisia zake ili muweze kwenda sawa. Usije ukasema hili nalo ni gumu kutekeleza.
Haya sasa, jiongeze inavyotakiwa. Tendo husika ni muhimu kwake. Mapozi yake ni sitaki nataka tu. Ni kweli wewe ndiye umemuanza lakini huduma hiyo naye anaihitaji kwa kiwango cha juu. Pale anaporidhia tu, hakikisha humuachii mpaka akiri mwenyewe kwamba ameridhika. Hili ni muhimu sana.
KUWA KIMYA/ KUTOONESHA HISIA KITANDANI
Unaweza kudhani kwamba kuzungumza kimahaba, kunena maneno ya shombo katikati ya shughuli, itakufanya uonekane usie na maana. Kama mawazo yako yamegota huko, utaendelea kupoteza ubora wa faragha kila siku iendayo kwa Mungu. Badilika.
Hata wewe mwenyewe, unapohusika na mwanamke mkimya, asiyezungumza chochote, hutajisikia vizuri. Basi kwa taarifa yako, naye pia atakereka kwa ukimya wako. Kuwa mcheshi kwenye tendo, mwaga pongezi panapotakiwa, kwa kifupi unatakiwa kuweka wazi hisia zako.
Tendo lenyewe halihitaji ukimya. Linataka mawasiliano ya hatua kwa hatua. Hutaonekana mjanja kwa sababu upo kimya. Hutaheshimiwa kwa kutoongea maneno ya shombo, zaidi utahesabika ni mshamba usiyejua chochote katika mapenzi, ikatae sifa hii ya kipuuzi.
Inawahusu pia wanawake kwa sababu wao ndiyo hutakiwa kutoa miguno na kuzungumza zaidi. Kama wako hujivika utulivu, haongei chochote mpaka chumba kinakuwa kimya wakati lipo jambo lenye maana zaidi linaendelea. Kataa ukimya kwa sababu ni adui wa penzi lenye mashamshamu.
Kuna ujinga ambao ni lazima kuuweka wazi hapa; kuna watu wengi huamini tendo la faragha ni la aibu, kwamba mtu mwenye heshima zake kulifanya haitoi picha nzuri. Imani hiyo ndiyo sababu ya wengi kufanya kama hawataki. Hili ni zaidi ya kosa la jinai.
Siyo tendo baya ndiyo maana lenyewe ndiyo sababu ya wewe kuwepo duniani. Ni burudani ya asili tena ya haki zaidi ambayo Mungu amemtunuku kila binadamu mwenye afya njema. Sasa basi, kufanya kama unajilazimisha, unakuwa unajifanyia ukatili wewe mwenyewe.
Kadhalika unalifanyia ukatili tendo lenyewe, vilevile unamkatili mwenzi wako. Ikiwa na yeye anajifanya bubu, gogo, kugeuka tabu, kujitikisa mvivu, kuguna hataki, kuongea mdomo kaweka gundi, hilo ni tatizo kubwa sana. Msiwe kimya ili mapenzi yalete maana kati yenu.
Mwanamke hudatishwa na hisia. Yale maneno ya shombo utakayoongea kipindi ‘muziki’ unaendelea ndiyo hasa humfanya aone raha. Mbona yeye akisema maneno yake wewe unafurahia, basi ujue siyo uchafu, wala usiite matusi. Katika eneo hilo yanaruhusiwa.
Juu ya kitanda, maneno kama “nipe mwongozo, tafadhali” na mengine yenye sura kama hiyo siyo mwafaka. Kama unafurahi ukisikia kinywa chake kinatema maneno ya shombo kusifia kazi yako, ujue naye atafurahi zaidi. Tuache nyenendo za kizamani.
Itaendelea wiki ijayo.
GPL
No comments:
Post a Comment