ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 10, 2013

MAONI YA BASALAMA KUHUSU UJIO WA MHE. MWIGULU NCHEMBA NCHINI MAREKANI

Mhe. Mwigulu Nchemba akiongea na Watanzania DMV kwenye ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryland pamoja na mambo aliyoongea ni kuwaomba Watanzania ughaibuni kupima wanayoongea wapinzani huku akisikitishwa na kauli za upinzani wanaodai barabara si maendeleo huku akitoa mfano wa barabara za Marekani ni kielelezo cha maendeleo ukilinganisha na barabara Tanzania.
Tulipokuwa kwenye mkutano wa watanzani Washington DC ambao ulihudhuriwa na miongoni mwa wageni waalikwa Mh. Mwigulu Nchemba na Rajabu Luhavi. Bwana Mmoja alimuuliza Mh.Luhavi maswali ambayo yote yalilenga kwenye wajibu wa serikali na haki ya maendeleo ya nchi. Zaidi kwa kudai mustakabali wa utendaji na kuilaumu Serikali imeshindwa kuleta maendeleo.

Yaliyoyangu ni kama ifuatavyo: Maendeleo ya aina yoyote yatakayo letwa na Serikali, ni lazima Serikali igharimike. Ili serikali iweze kuleta maendeleo, ni lazima matumizi ya pesa yapatikane. Pesa zinapotiwa kwenye chanzo, ndipo chanzo hicho huweza kuzaa kitu kinachoitwa maendeleo. Serikali ni chombo mbacho kinaanza na kutokuwa na pesa. Mfumo unaotumika na nchi ndio unaotafsiri utaratibu wa upatikanaji wa chanzo cha pesa za ujenzi wa msingi wa maendeleo. Serikali kama ya Tanzania ni Serikali ya kidemokrasia, hivyo inategemea utaratibu wa ukusanyaji taxi kutoka kwa watu wake (wananchi) ndipo inapata pesa za kupeleka kwenye chanzo cha maendeleo.

Mimi Nikamuuliza huyu bwana mwenye kudai maendeleo ya nchi na kuishutumu serikali kuwa haileti maendeleo. Pamoja na kutokusudia kwangu kuchukua jukumu la kujibu maswali hayo, lakini ningependa mchango wa huyu bwana katika Taifa hili tunalolijadili. Nikamuuliza Je? Yeye binafsi amewahi kulipa taxi tokea azaliwe. Baada ya maelezo mengi, huyu bwana akajinijibu kuwa hajawahi kulipa taxi hata mara moja. Nikamwambia huyu bwana kuwa kwa mtazamo wangu, yeye si katika wanaostahiki kuhoji maendeleo ya nchi.

Ukweli ni kwamba:
Kila Mtanzania anayeishi ndani ya Tanzania mwenye kuamka asubuhi na kufanya utaratibu wake wa maisha ya kila siku na kutoka sehemu A kuelekea sehemu be, huwa moja kwa moja anachangia nchi kupiga hatua moja nyuma. Hivyi basi jitihada inaitajika ya makusudi ya ima nchi ibaki pale ilipo au kupiga hatua moja mbele. Jitihada hii inapofanyika, na Mtazania huyu akawa si mwenye kushiriki ya jitihada hiyo, basi huwa ni mbadhilifu wa maendeleo. Na Zaidi ikiwa Mtanzania huyu ni mwenye kudai au kubeza jitihada hii, basi huyu huwa ni muhujuma wa maendeleo.

Mara nyingi haya hutokea sio kwa makusudi ila kutokana na kutokuwa na ufahamu wa kutosha wa majukumu yetu na wajibu wa kiraia. Wananchi wengi hawafahamu majukumu yao kama raia, na wamekuwa wakiamini tu kuwa Serikali ni jukumu lake kuleta maendeleo. Inawezekana kukawa na ukweli katika muono wa namna hii, lakini kuna nadharia inayoshabihiana ili fursa ya maendeleo iwepo, Nayo ni ushirika wa wananchi. Ushirika unapopatikana na chachu hizi zinakuwa katika kiwango cha kutekelezeka. Na bila shaka haki ya kudai kwa maendeleo inazidi kuwa na mantiki.

Nilipata fursa adhwim ya kuwa karibu na Mh.Rais Kikwete alipotembelea North bay, California. Alifanya Mkutano na Watanzania wa Oakland-CA, alifungua Ofisi ya Balozi wa hiyari ya Ahmed Issa Al’Qasmy hapo San Rafael na chakula cha jioni, alitembelea mji wa Vallejo na Sister City pamoja na chakula cha mchana. Katika mikutano mitatu hii, katika mambo ambayo aliyazungumza ni pamoja na maendeleo ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Vilevile katika msafara mwingine ambao ulikuwa katika nyakati zinazowiana ni wa Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, ambao akiongozana na Mh.Rajab Luhavi. Pia nilipata fursa ya kuhudhuria mikutano ya California, North Carolina na Washington-DC. Katika jambo ambalo lilinigusa sana ni pale ambapo Mh. Mwigulu kwa ufasaha aliweza kufasiri, kuchambua na kutolea maelezea ya kina juu ya mengi ambayo Serikali hii imeweza kuyafanya. Na pia kutoa fursa ya watu kuuliza maswali yote, mkapa maswali yakaisha. Mwisho wa mkutano kila mmoja akaonekana kufarijika vya kutosha.

Katika jambo ambalo nililiona pia, viongozi wote hawa waliweza kuliweka wazi na kuwaelimisha Watanzania juu ya wajibu wao na jinsi gani wanaweza kushiriki katika maendeleo au ujenzi wa Taifa letu.

Naamini utaratibu huu ukiendelea kuhabarishana, kuelimishana kati ya serikali na wananchi, wananchi na wananchi

5 comments:

Anonymous said...

Basalama huna mpya...umekuja DMV ukijinadi kuwa wewe ni katibu wa kukusanya maoni ya katiba lakini ukweli ni kwamba wewe ulikuwa na ajenda ya siri ya kupotosha maoni yetu kuhakikisha yanafanana na Sera za ccm ambao wanajaribu kila wanachoweza kuhodhi rasimu ya ukusanyanyi. Pili, kila mtanzania alieuliza swali amefanya vile kwa mapenzi ya nchi na Kama kiongozi analalamika juu ya aina ya maswali basi huyo kiongozi hatufai... Ni wajibu wake kujibu maswali na Kama maswali yanamtoa raha ni bora atafute kazi nyingine. Tumechoshwa na viongozi waongo na wanaofikiria sote ni lazima tufikili kama wao.

Anonymous said...

asante sana mdau kwa maelezo mazuri.!!..lakini mdau mbona hujajiuliza mwenyewe kwanza swali la kwanini watu wamefikia kuishutumu tu serikali??

..ni hivi ndugu yangu hizo kodi unazosema watu hawatoi ni sababu hata zile ndogo zinazotolewa ZINATAFUNWA!.na hii ndio inayoamsha hasira zote za watu kulaumu tu..kuna mambo mengi kama wizi wa fedha za EPA, kuficha hela Uswisi, mikataba tata, etc..kama serikali ingewachukulia hatua stahiki hao wanaofanya haya maovu basi watu wangekuwa na imani na kutoa zaidi hizo kodi tena kwa hiyari..!.

Kitu kinachowafanya watu watoe kodi vizuri nchi yoyote duniani ni pale wanapoona kodi inatumika vizuri bila kupotea. Ungekuwa unaelewa vizuri ndugu yangu ungehoji hata safari ya mh rais wetu huko kwenye maeneo yote uliyoyataja kama ni sahihi sana kwa mtu wa level yake au ameshauriwa vibaya...maana gharama za kufanya president a-move from one place to another ni kubwa sana kuliko labda angewakilishwa na balozi au hata waziri ukizingatia nchi yetu bado ni maskini sana na kutegemea misaada!

Hivyo ndugu jenga mtazamo wa kujiuliza maswali magumu binafsi kwa kila unaloliona na si kuliangalia tu kwa nje!

James
Ujerumani

Anonymous said...

Basalama na huyo uliyemuuliza wote hamuelewi mnachowasilisha...Hivi huyo mtu atawezaje kusema hajawahi kulipa KODI ilhali alizaliwa Tanzania? Hivi hamtambui kodi inalipwaje? Tuache ushabiki wa kisiasa na tuchangie mada zitakazoikomboa Tanzania. Duania hii imejaa UONGO kuliko ukweli sababu ya watu kama BASALAMA...mnapotosha ukweli ili mjenge hoja potofu za kuunga mkonoupuuzi mwingi unaofanywa na serikali, kwa kweli inasikitisha..

Anonymous said...

ndugu Basalama kwanza nikupe hongera kwani umetumia uhuru wako vizuri wa kuongea kwasababu unapependa kuongea.
lakini nasikitika unaongea bila kufikri wala utafiti.Hivyo unajimaliza katika uwanja wa kisiasa wala hauna hoja unayochangia.wewe tueleze unachangia nini sio kuhoji swali la mtu mchango wako ni nini kujenga Tanzania?Kama unaomba kazi ccm na basi omba kazi lakini siasa huna.Nakubaliana na aliyesema aliyeuliza swali na wewe wote mko sawa.kama amezaliwa tazania analipa kodi lakini haelewi tu ni kama wewe.

Anonymous said...

Ccm oyeee au cuf oyeee????