Meya wa Ilala Jerry Slaa anatarajia kuazindua mpango mpya katika shule za msingi ndani ya Ilala ambao umepewa jina la “Mnazimkinda”. Program hii itasaidia wanafunzi kutambua na kukuza vipaji vyao hasa kwenye kuimba,kucheza mpira,kuruka kamba,kukimbia na aina nyingine ya michezo.Lengo kubwa la mpango huu ni kusaidia kuongeza mahudhurio ya wanafunzi shuleni, kuchangamsha mwili na akili zao na pamoja na program zitakazosaidia kujua kuandika na kusoma vizuri.
Meya Jerry Slaa amesema, “Mnazimkinda lengo lake kubwa ni kusaidia wanafunzi wa shule za msingi ndani ya Ilala kuongeza uwezo wao wa kusoma, kuandika,kujiamini,kuongeza mahudhurio shuleni na mwisho kufikia malengo ya taifa kwa wanafunzi hawa kupata matokeo mazuri. Program hii itawafanya wanafunzi wapende shule na elimu kwa ujumla”.
Pia aliongeza kwamba mpango huu utazinduliwa mwezi huu kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na siku hiyo itashereheshwa na wasanii ambao walisoma shule za Ilala kwenye miaka iliyopita.

2 comments:
Wazo zuri lakini mwelekeo sio.
Yako wapi mashindano ya kutafuta kipaji cha mahesabu, uvumbuzi wa kisayansi au katika sanaa kama vile ushairi, matumizi ya lugha nk???
Ubunifu wetu ni kwenye kuimba na kucheza tu? Kwangu, usanii wa kisasa umekuwa ndio chimbuko kubwa la mmonyoko wa maadili.
Mhe. Silaa ni kati ya viongozi vijana ninao wa admire sana.
Unayo potential ya kufikia kilele cha ngazi za siasa. Kwa hili sikuungi mkono. Kuna umuhimu wa kuhamasisha watoto hawa kuhusu vipaji vyao vingine zaidi ya kucheza mpira na kuimba Bongo flava.
Kwa sababu wakijuwa tu wanakipaji cha kuimba..... Shule ndio bye bye.
Itakuwa unawaonyesha njia ya kukimbia darasa.
Huu ni muono wangu.
This is what we need "fresh blood, mind and actions". Sio wazee wasio na mawazo fresh. UMISETA IRUDI PLEASE. Watu tulikuwa tunasafiri mkoa hadi mkoa kwenye michezo na ilikuwa inatupa discipline ya kujituma kama hufanyi vizuri darasani huwezi kuwa mwamamichezo! It was that simple ndo maana watu tulifahamiana sana miaka hiyo from DAR TO ARUSHA mnajua kina nani ni wakali wa netball, basketball, soccer kukimbia na ilikuwa inafanya shule ziwe more fun to be na mahudhurio mazuri, ukiwa mtoro hakuna kwenda kwenye michezo. THERE WERE ACCOUNTABILITY IN EVERYTHING WE DID!
Post a Comment